banner68
banner58

Ajibu awapa ujumbe mzito waliomsema kwa kutokwenda Algeria

Ajibu awapa ujumbe mzito waliomsema kwa kutokwenda Algeria

06 May 2018 Sunday 11:22
Ajibu awapa ujumbe mzito waliomsema kwa kutokwenda Algeria

Na Amini Nyaungo

Nyota wa Yanga Ibrahimu Ajibu amefanikiwa kupata mtoto wa kike leo, jambo ambalo ni jibu zuri kwa waliokuwa wanamlaumu kwa kutosafiri na timu yake kwenda nchini Algeria wiki hii.

Ajibu hakuweza kusafiri na Yanga ambayo imeelekea Algeria kwa ajiri ya mchezo wa kombe la Shirikisho nchini humo leo.

Mashabiki wa Yanga wamekuwa wakiongea na kuhoji huku wengine kumtupia lawama mchezaji huyo kupitia kurasa zake za mitandao ya jamii wakitoa matusi wengine kuhoji kwanini hakwenda na timu.

Taarifa ya Katibu mkuu wa Yanga kuhusu kutojumuishwa kwa Ajibu katika kikosi hiko inadhihirisha kuwa kweli lisingekuwa jambo zuri kumwacha mke wake ambaye alikuwa katika hatua ya mwisho ya kujifungua.

Mkwasa alisema kuwa Ajibu ameachwa kwa kuwa na matatizo ya kifamilia na hili linathibishwa kuwa ni kweli.

Maneno ya Ajibu kupitia ukurasa wa Instagram wa Yanga amewashukuru na kumshukuru Mungu kwa kumpatia zawadi ya mtoto huku akiwasamehe wote waliombeza.

"Namshukuru Mungu ametujali kupata mtoto wa kike, hapo kabla nilikuwa na hofu kubwa kwa sababu ujauzito wa mke wangu ulikuwa na matatizo mengi, kuna wakati nilikuwa na hofu kubwa juu ya maisha yake. Naumizwa na wanaonishambulia kupitia sms kuwa nimegoma kuichezea timu, sina sababu ya kufanya hivyo. Mpira ni kazi yangu," amesema.

Mwisho amemalizia kusema amewasamehe na kuwa kitu kimoja katika timu.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Willy Akyoor 2018-05-08 16:30:03

Ongera Ajibu kwa kupata mtoto wa kike

Avatar
sospeter 2018-09-14 11:21:15

hongera mzee baba