Algeria bingwa mpya Afcon 2019

Algeria bingwa mpya Afcon 2019

20 July 2019 Saturday 06:28
Algeria bingwa mpya Afcon 2019

Cairo, Misri

Algeria imeshinda kombe la mataifa ya Africa kwa mara ya pili baada ya kuifunga Senegal katika fainali iliyochezwa usiku wa Julai 19, 2019  mjini cairo.

Shambulio la mapema la  dakika ya pili ya kipindi cha kwanza  la mchezaji Baghdad Bounedjah lilimgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kupita juu ya mlinda langgo Alfred Gomis

Senegal, ambao hajawahi kushinda michuano hiyo , walipata penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira katika kipindi cha pili lakini refa wa video VAR alibadilisha uamuzi huo na kusema penalti haikufaa kutolewa

Algeria ilitumia kila mbinu kuwazuia wachezaji wa Senegal waliofanya mashambulizi ya kila aina ili kushinda kombe hilo tangu 1990.

Senegal ambao walikuwa wakishiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002 , walitawala kipindi kikubwa cha mechi lakini wakashindwa kuzalisha matunda.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.