banner68
banner58

Alliance FC watoa tahadhari kwa Yanga

Waahidi kuipa furaha Simba

Alliance FC watoa tahadhari kwa Yanga

Waahidi kuipa furaha Simba

11 October 2018 Thursday 06:34
Alliance FC watoa tahadhari kwa Yanga

Uongozi wa timu ya Alliance FC umejipanga vilivyo kuelekea mechi yake na Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kupigwa Oktoba 20 kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Alliance wamesema kuwa wameshaanza maandalizi ya moto kuelekea mechi hiyo ambayo wametamba kuweka historia jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa timu hiyo, Jackson Mwafulango, amesema wamejipanga kuifunga Yanga iki kuweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kuchukua alama tatu za Yanga msimu huu.

Mafulango amejigamba kuwa watakuja na moto wa aina yake ili kuwashangaza wengi ambao wanaichukulia timu hiyo kuwa ni ya kawaida.

"Tumeshaanza maandalizi muda na tunataka kuja kuondoka na alama tatu dhidi ya Yanga OktobA 20, tumedhamiria kuweka rekodi ya kuondoka na alama hizo ili kuweka rekodi ya kuwafunga Yanga msimu huu" alisema.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.