Amri Said Kocha Mpya Lipuli

Amri Said ni beki wa zamani wa Majimaji ya Songea na Simba SC

Amri Said Kocha Mpya Lipuli

Amri Said ni beki wa zamani wa Majimaji ya Songea na Simba SC

04 June 2018 Monday 20:05
Amri Said Kocha Mpya Lipuli

Na Habakuki Urio

TIMU ya Mbao FC ya Mwanza leo imeingia mkataba wa mwaka mmoja na kocha Amri Said ‘Stam’ kuifundisha timu hiyo kwa msimu ujao.

Mkataba huo umesainiwa leo kwenye ofisi za wadhamini wakuu wa Mbao FC, GF Trucks &Equipment Limited, Vingunguti mjini Dar es Salaam na kushuhudiwa na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Imran Karmali.

Na ni Mwenyekiti wa Mbao FC, Solly Zephania Njashi aliyesaini mkataba huo na Amri Said leo mjini Dar es Salaam.

Amri Said, beki wa zamani wa Maji Maji ya Songea na Simba SC ya Dar es Salaam anachukua nafasi ya kocha wa muda Fulgence Novatus aliyekuwa anaiongoza timu hiyo baada ya kuondokewa na aliyekuwa kocha wake Mkuu, Mrundi Etienne Ndayiragijje.

Ndayiragijje ambaye aliiongoza kwa mafanikio Mbao FC kwa msimu mmoja na nusu ikiwemo kuifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) amejiunga na Timu ya Manispaa ya Kinondoni (KMC).

Amri anajiunga na Mbao FC akitokea Lipuli ya Iringa ambako alikuwa kocha Msaidizi mbele ya Suleiman Matola mchezaji mwenzake na Nahodha wake wa zamani SImba SC.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.