Angalia safari ya Singida United na Mtibwa Sugar hadi fainali leo

Kabla ya kuelekea fainali hiyo kila kitu kimeandikwa na hii ni safari ya Singida United na Mtibwa hadi kufikia hatua ya fainali

Angalia safari ya Singida United na Mtibwa Sugar hadi fainali leo

Kabla ya kuelekea fainali hiyo kila kitu kimeandikwa na hii ni safari ya Singida United na Mtibwa hadi kufikia hatua ya fainali

02 June 2018 Saturday 11:17
Angalia safari ya Singida United na Mtibwa Sugar hadi fainali leo

Na Amini Nyaungo

Finali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Tanzania inayofahamika kama ‘Azam Sports Federation Cup’ ambayo itafanyika leo huku Singida United ikiwa uso kwa uso na Mtibwa Sugar katika dimba la Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Kabla ya kuelekea fainali hiyo kila kitu kimeandikwa na hii ni safari ya Singida United hadi kufikia hatua ya fainali.

Singida United dhidi ya Green Worriors

Katika mchezo huo matokeo yalitoka sare ya 0-0 ambapo Singida ilishinda kwa penati 4-3.

Singida United dhidi ya Polisi

Hii sasa wameshinda 2-0 na kukata tiketi kuingia nusu fainali na kukutana na mabingwa wa zamani wa kombe hilo Yanga.

Singida United dhidi ya Yanga

Mchezo huu ulivuta hisia za watu wengi hasa kiongozi wa juu wa Singida United hasa kutokana na ukweli kwamba kiongozi wa juu timu hiyo Mwigulu Nchemba ni shabiki lialia wa Yanga. Matokeo ya mwisho baada ya dakika 90 yalikuwa sare ya 1-1 hapo sasa ndipo SIngida walipoitungua Yanga kwa penati 4-2.

Safari ya Mtibwa nayo haikuwa rahisi ndani yake kulikuwa na ugumu wake.

Haikuwa rahisi ilianza na timu za ligi za mikoa baadae mechi kali ilikuwa baina yake na Azam ambapo matokeo yake yaliamuliwa kwa mikwaju ya penati baada ya matokeo ya uwanjani kuwa ni sare ya 0-0. Mitbwa iliua penati 9-8.

Mtibwa Sugar dhidi ya Stand United

Mchezo huu uliikuta Mtibwa ikiwa kwenye ubora wake, hivyo kupata ushindi wa magoli 2-0 na hatimaye kutinga fainali.

Je unahisi timu gani itachukua ubingwa wa michuano hiyo kwa mara ya kwanza kwa upande wa timu hizo?

Unaweza kuungana nasi katika mitandao yetu ya kijamii Instagram Twitter na Facebook tunatumia Azaniapost.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
marindi 2018-07-13 18:28:53

0686741496