banner68
banner58

Angalia Simba hii na vikosi vitatu tofauti ‘watapata taabu sana’

Simba ya msimu ujao inaonekana kukamilika kila idara, huku kila mfumo na kikosi kitakachopangwa kuonekana tishio

Angalia Simba hii na vikosi vitatu tofauti ‘watapata taabu sana’

Simba ya msimu ujao inaonekana kukamilika kila idara, huku kila mfumo na kikosi kitakachopangwa kuonekana tishio

27 June 2018 Wednesday 12:24
Angalia Simba hii na vikosi vitatu tofauti ‘watapata taabu sana’

Na Amini Nyaungo

Kwa washambuliaji wanne wa Simba na kikosi chao kilivyo sasa inaweza kuleta mifumo mitatu tofuati na wachezaji tofuati.

Kikosi cha kwanza cha wekundu hao wa Msimbazi kinaweza kutumia mfumo wa 4:4:2 ambapo golikipa katika kikosi cha kwanza Aishi Manula, kulia anacheza Kapombe kushoto Kwasi beki wa kati wakiwa ni Serge Wawa na Erasto Nyoni.

Kiungo ya kati ni Jonas Mkude akiwa sambamba na Kotie, huku Niyonzima akisimama katika Shimo namba kumi, wakati huo Okwi shavu la kushoto na Kichuya shavu la kulia.

Katika mfumo wa 4:4:2 kumbuka wanakaa wanne nyuma wanne kati na wawili mbele.

Washambuliaji Meddie Kagere pamoja na John Bocco hapo shughuli inakuwa imemalizika kwa kikosi cha kwanza.

Katika kikosi cha pili ambacho unaweza kutumia 4:3:3 hapo sasa ndio shughuli inakuwepo.

Sehemu ya nyuma itabaki vile vile huku kiungo kitabadilika kidogo, atakaa Jonas Mkude, James Kotei pamoja na Niyonzima.

Huku sehemu ya mbele Meddie Kagere, John Bocco na Emanuel Okwi hapo sasa ndio balaa.

Katika kikosi kinachofuata cha akiba ambacho pia kitachezwa kwa mfumo wa 3:5:2.

Kipa atakaa Said Mohamed Nduda, ukuta utakuwa Mlipili, Kwasi pamoja na Kapombe.

Sehemu ya kiungo itakuwa Mzamiru Yassin, James Kotei, Haruna Niyonzima na Shiza Kichuya.

Wawili wa mbele Adam Salamba pamoja na Marcel Kaheza, unaonaje kikosi hiki?

Kuna wachezaji wengine wa kikosi cha kwanza nimewachomeka katika kikosi hiki maana hakiwezi kuchezwa na wasiopata namba pekee.

Unaweza kujadili kupitia kurasa zetu za Instagram, Twitter na Facebook utuambie umekionaje kikosi hiki cha Simba katika msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Goodruck 2018-07-23 11:27:12

Simba wasihangalie majina yoyote apewe nafasikama mchezaji

Avatar
Paschal Henry 2018-06-28 10:22:42

Kikosi kiko vizuri sana ila ombi langu kocha djuma aachiwe timu maana anaweza pia anawapatia wachezaji wote nafasi ya kucheza

Avatar
Gotard mapunda 2018-07-14 16:26:06

simba nawaomba wanisajili katika kikosi b

Avatar
ISACK MSENGI 2018-07-21 21:18:45

NAMI NAPONGEZA HATUA ZOTE ZA KIKOSI

Avatar
Simba giant 2018-07-23 09:33:10

Watapata tabu sana 2

Avatar
LYOCHI SAID 2018-07-25 11:14:55

simba oheeeeeee

Avatar
OYOO! 2018-07-26 20:02:51

OYOO!

Avatar
SHAIBU MKUMBANGI 2018-07-27 23:16:29

Jamani wanasimba tuwe makini tuakikishe tuna toa tena taji kama alivo sema kocha kila mchezeji awe anapewa nafasi ya kucheza.