Arsenal yafufua matumaini kwa CSKA Moscow

Mfaransa Alexandre Lacazette aliyefunga magoli mawili

Arsenal yafufua matumaini kwa CSKA Moscow

Mfaransa Alexandre Lacazette aliyefunga magoli mawili

06 April 2018 Friday 19:05
Arsenal yafufua matumaini kwa CSKA Moscow

Na Amini Nyaungo

Arsenal imejiwekea matumaini ya kusonga hatua ya nusu fainali ya michuano ya Europa ndogo baada ya kuifunga CSKA Moscow ya Urusi kwa jumla ya magoli 4-1.

Mfaransa Alexandre Lacazette aliyefunga magoli mawili pamoja na kiungo wa Wales, Aaron Ramsey aliyefunga magoli mawili.

Mturuki aliyebadili uraia na kuitumikia Ujerumani, Mesut Mustafa Ozil naye ameibuka baada ya kutoa pasi zilizozalisha magoli mawili katika mchezo huo ambao ulikuwa mzuri wa washika bunduki wa jiji la London.

TAKWIMU KATIKA MCHEZO HUO

Granit Xhaka amepiga pasi sahihi 66 katika mchezo huo huku beki Shkodrn Mustafi amesaidia kuokoa nafasi 7 za wazi longoni mwa Arsenal.

Arsenal imemiliki mpira kwa 57% wakati wageni walimiliki kwa 43%, jumla ya mashuti ambayo Arsenal wameyapiga 18 huku CSKA Moscow wakipiga 11. Katika hayo mashuti kwa upande wa Arsenal yaliyolenga goli 9 huku CSKA Moscow 4

Pasi sahihi 480 huku wageni wakipiga pasi 334, hivyo Arsenal waliongoza kwa kupiga pasi sahihi 84% kwa 79% za CSKA Moscow.

Faulo 11 kwa Arsenal na 14 kwa CSKA Moscow huku washika bunduki wa London wakizidiwa kwa kona ambapo walipata kona 3 wakati CSKA Moscow 4. Kona 7 huku ‘offside’ zikiwa 7 kwa Arsenal na 5 kwa CSKA Moscow.

Mchezaji bora wa mechi hiyo ‘Man of the Match’ akitajwa Ozil kwa namna alivyoweza kucheza na kutoa pasi za msaada bili huku pasi mbili nyingine akitengeneza za wazi wafungaji wakishindwa kutumbukiza kimiyani.

Matokeo mengine hapo jana Atletico Madrid imeshinda 2-0 dhidi ya Sporting CP,Lazio wakiwafunga Salzburg huku RB Leipizig ya Ujerumani ikiifunga Mareseille 1-0.

Kikosi cha Arsenal kilikuwa, Petr Cech, Bellerin,Monreal,Mustafi,Koscielny,Xhaka,Ramsey, Jack Wilshare,Mkhitaryan ,Ozil na Lacazette.

Kikosi cha CSKA Moscow, Akinfeev, Sergei, Aleksei,Vasili,Natcho,Dzagoev,Georgi,Aleksandr,Konstanti,Pontus and Ahmed Musa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.