banner68

Arsenal yaikabili CSKA Moscow, timu iliyoishinda mwaka 2006

Ni mara ya kwanza kwa timu ya Arsenal kuingia katika hatua ya robo fainali kwa michuano ya Ulaya tangu msimu wa 2009-2010

Arsenal yaikabili CSKA Moscow, timu iliyoishinda mwaka 2006

Ni mara ya kwanza kwa timu ya Arsenal kuingia katika hatua ya robo fainali kwa michuano ya Ulaya tangu msimu wa 2009-2010

05 April 2018 Thursday 13:53
Arsenal yaikabili CSKA Moscow, timu iliyoishinda mwaka 2006

Na Mwandishi Wetu

Arsenal wataikaribisha CSKA Moscow katika uwanja wa Emirate leo majira ya 4.45 usiku katika michuano ya UEFA ndogo.

Arsenal ina wasiwasi wa kumkosa Danny Welbeck ambaye ameanza mazoezi, ila anaonekana hayuipo safi `Doubtful` pamoja na Petr Cech huku Santiago Cazorla hatokuwepo kabisa katika kikosi hicho.

CSKA Moscow watakosa huduma ya wachezaji watatu, Mario Fernandez,Viktor Vasin na Kirill Nababkin ambaye ana kadi nyekundu.

Arsenal itaongozwa na Arsene Wenger ambaye tayari amefundisha misumu 21 huku akitunukiwa tuzo na Malkia Elizabeth wa Uiengereza shahada ya ufanyaji kazi bora katika nchi yake, CSKA Moscow wataongozwa na kocha Viktor Goncharenko. Muamuzi wa mchezo huu Pavel Kralovec kutoka Czechoslovakia.

Timu hizi zilikutana mwaka 2006 katika hatua ya makundi ambapo mchezo wa kwanza uliofanyika England walitoa sare ya bila kufungana mchezo wa pili Arsenal walipoteza 1-0.

Ni mara ya kwanza kwa timu ya Arsenal kuingia katika hatua ya robo fainali kwa michuano ya Ulaya tangu msimu wa 2009-2010 walipotolewa dhidi ya Barcelona.

`Gunners` haijawahi kupoteza hatua ya kwanza katika michuano ya Ulaya tangu 1972 ilipocheza dhidi ya Ajax ya Uholanzi.

CSKA Moscow hii ni mara yao ya tatu kuingia katika hatua hii katika historia ya timu hiyo tangu kuanzishwa.

Arsenal katika michezo yao mitano ya mwisho wamepoteza mmoja na kushinda minne , wakati CSKA Moscow pia wamepoteza mmoja na kushinda mine.

Azania Post

Updated: 05.04.2018 14:12
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.