Aveva, Kaburu mambo bado

Aveva, Kaburu mambo bado

21 September 2019 Saturday 06:30
Aveva, Kaburu mambo bado

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

MKURUGENZI wa Mashtaka nchini (DPP) amekata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwaondolea kosa la utakatishaji fedha aliyekuwa rais wa klabu ya Simba SC, Evance Aveva na makamu mwenyekiti wake Godfery Nyange (Kaburu).

Hatua hiyo imepelekea watuhumiwa hao wawili kushindwa kuachiwa kwa dhamana. Mshtakiwa mwengine katika kesi hiyo ni aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Zackaria Hanspope.

Septemba 19, 2019 washtakiwa hao waliondolewa kosa la utakatishaji fedha baada ya mahakama hiyo kutowakuta na kesi ya kujibu katika kosa hilo isipokuwa mengine saba.

Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amemueleza Hakimu Mkazu Mkuu Thomas Simba kuwa upande wa mashtaka umekata rufaa ya kupinga uamuzi uliotolewa Septemba 19, 2019 na mahakama hiyo.

Wankyo ameieleza mahakama hiyo kuwa upande wa mashtaka haujajiandaa kutoa hoja juu ya rufaa hiyo, hivyo ameomba kuahirishwa hadi siku nyengine.

Hata hivyo, Wakili wa utetezi Nehemia Nkoko ameieleza mahakama kuwa upande huo upo tayari kwa utetezi na kwamba wao walikuwa mahakamani hapo tangu asubuhi sambamba na mashahidi wao.

Nkoko ameeleza kuwa upande wa Jamhuri ulikuwa na notisi ya rufani tangu asubuhi wangeweza kuwasilisha hoja zao.

Nkoko ameeleza kuwa upande wa Serikali haujapinga dhamana ya washtakiwa na kwamba ilishatolewa tangu Septemba 19.

Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili Hakimu Simba amesema kuwa misingi ya mahakama ni kusikiliza na kwamba itakuwa haijautendea haki upande wa Jamhuri kwenye rufaa yao.

Amesema Septemba 23, 2019 atasikiliza hoja za upande huo siku na kwamba hajafuta dhamana ya washtakiwa ambao walirejeshwa mahabusu.

Septemba 20, 2019 washtakiwa hao walitarajiwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini bondi ya milioni 30 kwa kila mmoja.

Updated: 21.09.2019 06:35
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.