Aveva, Kaburu wakubali yaishe

Aveva, Kaburu wakubali yaishe

12 October 2019 Saturday 06:16
Aveva, Kaburu wakubali yaishe

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam.

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeelezwa kuwa aliyekuwa rais wa Simba SC, Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Kaburu wameandika barua kwa Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP).

Wakili wa Serikali Wankyo Simon amesema lengo ni kutaka kuanza majadiliano ya namna ya kuimaliza kesi hiyo.

Hata hivyo, leo Oktoba 11, 2019 washtakiwa wote walifika mahakamani na kesi ilipangwa kutolewa uamuzi kuhusiana na hoja mbalimbali zilizowasilishwa na upande wa mashtaka kuhusu mahakama kuwaondolea mashtaka ya utakatishaji washtakiwa hao.

Baada ya kuelezwa hayo,Hakimu Simba amesema bado hajamaliza kuandaa kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 18, 2019 ambazo atautoa uamuzi huo.

Hatua hiyo ilifikiwa na upande wa mashtaka baada ya mahakama kuwaondolea mashtaka mawili ya utakatishaji, kati ya kumi yaliyokuwa yakiwakabili Aveva na Nyange Kaburu baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka hayo dhidi yao.

Hata hivyo washtakiwa hao pamoja na mwenzao Zacharias Hanspope walikutwa na kesi ya kujibu katika mashtaka saba ambayo ni kughushi, kula njama, matumizi mabaya ya madaraka, kutoa nyaraka za uongo, na kutoa maelezo ya uongo ambayo upande wa mashtaka umeweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa

Kufuatia kuondolewa kwa mashtaka hayo ya utakatishaji washtakiwa wamepatiwa masharti ya dhamana kwa sababu mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliwanyima dhamana hayapo

Kwa mujibu wa uamuzi huo umetolewa na Hakimu Simba alisema ni jukumu la upande wa mashtaka kuthibitisha mashtaka yote kwa washitakiwa na kila shtaka linatakiwa kuthibitishwa peke yake na sio kwa kutegemeana.

Baada ya kuchambua ushahidi wa mashahidi 10 wa upande wa mashitaka, ukiacha shtaka la tano na sita mahakama iliona kuwa washtakiwa wanakesi ya kujibu katika shtaka la 1,2,3,4,7,8 na 9 isipokuwa katika shtaka la tano na sita ambayo ni ya utakatishaji yaliyoondolewa.

Kufuatia kuondolewa kwa mashtaka hayo, Wakili wa washtakiwa hao Nehemia Nkoko aliiomba mahakama kuwapatia wateja wake dhamana kwani mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo yaliyokuwa yanawanyima dhamana hayapo.

Wakili wa Takukuru, Leornad Swai alipoulizwa kama anapingamizi lolote juu ya dhamana alidai hawana pingamizi.

Hakimu Simba aliwapatia masharti ya dhamana washtakiwa ya kuwa na wadhamini waili watakaosaini bondi ya Sh 30 Milioni kwa kila mmoja pamoja na kuwa na vitambulisho

Katika shtaka la kwanza, Aveva na Kaburu wanadaiwa kula njama ya kutenda kosa la matumizi mabaya ya madaraka.

Katika shtaka la pili la Aveva na Kaburu wanadaiwa kutumia vibaya madaraka yao kwa kuandaa fomu ya kuhamisha fedha Dola za Kimarekani 300,000 kutoka kwenye akaunti ya Simba iliyoko benki ya CRDB Azikiwe kwenda kwenye akaunti binafsi ya Aveva iliyoko benki ya Barclays.

Katika shtaka la tatu Aveva na Kaburu wanadaiwa kwa pamoja kughushi nyaraka iliyokuwa ikionesha Simba inalipa mkopo wa USD 300,000 kwa Aveva kitu ambacho sio kweli.

Pia Katika shtaka la nne Aveva anadaiwa katika banki ya CRDB anadaiwa kutoa nyaraka ya uongo ikionesha Simba wanalipa mkopo wa USD 300,000

Aveva anadaiwa kuwa katika Benki ya Baclays Mikocheni alijipatia USD 187,817 wakati akijua zimetokana na kughushi.

Katika shtaka la sita, Kaburu anadaiwa kumsaidia Aveva kujipatia USD 187,817 kutoka kwenye akaunti ya Simba wakiwa wanajua fedha hizo zimetokana na zao la kughushi.

Aveva, Kaburu na Hans Poppe wanadaiwa kughushi hati ya malipo ya kibiashara wakionesha kwamba nyasi bandia zilizonunuliwa na Simba zina thamani ya USD 40,577 huku wakijua kwamba siyo kweli

Katika shtaka la nane, Aveva anadaiwa kuwasilisha hati ya malipo ya kibiashara ya uongo kwa Levison Kasulwa kwa madhumuni ya kuonesha kwamba Simba wamenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577

Shtaka la tisa, Aveva, Kaburu na Hanspope wanadaiwa kuwasilisha nyaraka za uongo kuonesha kuwa Simba imenunua nyasi bandia zenye thamani ya USD 40,577.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.