Aveva, Kaburu wapata dhamana, waanza kujitetea

Aveva, Kaburu wapata dhamana, waanza kujitetea

19 September 2019 Thursday 17:04
Aveva, Kaburu wapata dhamana, waanza kujitetea

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA Rais wa Klabu ya Simba SC, Evans Aveva na makamu wake Godfrey Nyange maarufu Kaburu wamedhaminiwa na kuruhusiwa kurejea nyumbani. Hata hivyo leo Septemba 20, 2019 wataanza kujitetea.

Pia wamefutiwa shtaka la kutakatisha fedha baada ya washtakiwa kuonekana hawana kesi ya kujibu katika shtaka hilo. Kabla walikuwa wakikabiliwa na mashtaka 8

Uamuzi huo ulitolewa Septemba 19, 2019 na  Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Thomas Simba na kwamba washtakiwa walitakiwa wadhaminiwe na wadhamini wawili watakaosaini dhamana ya maandishi ya milioni 30, wadhamini wawe na vitambulisho. Washitakiwa hao walitimiza masharti ya dhamana.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi  leoSeptemba 20, 2019 ambapo washitakiwa hao akiwamo aliyekuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu ya ,Simba SC Zachariah Hans Pope wataanza kujitetea

Updated: 20.09.2019 05:50
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.