Baada ya dili kwenda Levante kusuasua, Samatta sasa kwenda klabu hii England

Baada ya dili kwenda Levante kusuasua, Samatta sasa kwenda klabu hii England

01 August 2018 Wednesday 13:14
Baada ya dili kwenda Levante kusuasua, Samatta sasa kwenda klabu hii England

Achana na habari za La Liga. Straika namba moja wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta anaweza kuwashangaza mashabiki wake kwa kutua Ligi Kuu ya England muda wowote kuanzia sasa.

Baba mzazi wa mchezaji huyo tajiri zaidi nchini, Mzee Ally Samatta amefichua siri kubwa aliyoelezwa na mwanae huyo kuwa yupo katika mipango mizito ya kujiunga na timu mbili za England ambazo ni Leicester City na West Ham United, huku akisisitiza lolote linaweza kutokea.

Samatta mwenye miaka 25, anayekipiga katika kikosi cha KRC Genk cha Ubelgiji, alitua hapo Januari, 2016 akitokea TP Mazembe ya DR Congo.

Akizungumza na Championi Jumatano, Mzee Samatta alisema kuwa licha ya mtoto wake kudaiwa kutakiwa na Levante, lakini kwa upande wake alimdokeza ana mpango wa kwenda Leicester City kutokana na kushawishiwa na rafiki yake waliocheza wote Genk kabla ya kutimkia timu hiyo, Wilfred Ndindi.

“Kiukweli hizo taarifa nimezisikia kama watu wengine wanavyosema kwamba sijui hao Levante ya Hispania, wengine wanaitaja Borussia Dortmund ya Ujerumani kuwa nao pia wamekuwa wanamuhitaji, lakini mimi nimeongea naye mwenyewe na alichosema ni kwamba kama mimba ndiyo imetunga basi tusubiri tuone kitakachotokea,” alisema Mzee Samatta na kuongeza.

“Uzuri Samatta kuna watu ndiyo wanamsimamia na hata hilo suala la Levante ndiyo maana akasema tusubiri kitakachotokea kwa sababu mwenyewe yupo kwenye mipango ya kwenda England na timu nilizoambiwa ni Leicester na West Ham lakini Leicester ndiyo sana kwa sababu pale kuna rafiki yake kutoka Nigeria, Wilfred Ndidi ambao walicheza pamoja Genk ila amenisisitiza kwamba atakayekuwa na kisu kikali ndiye atakula nyama.”

Mpaka sasa akiwa na Genk, Samatta amecheza jumla ya mechi 54, za Ligi Kuu Ubelgiji pamoja na michezo 12 ya mashindano ya Europa Ligi.

Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa Samatta kutokana na kusumbuliwa na goti jambo lililomfanya acheze mechi 35, lakini msimu huu yupo fiti na tayari ameanza kazi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
MHINA .D. 2018-08-19 08:30:52

KIUKWELI TOKA MOYONI MIMI NAMUOMBEA SANA DOGO SAMATA,ILA APAMBANE AENDE UINGEREZA ILI TUMUONE,PIA AJUE KUA SPAIN KODI NIKUBWA

Avatar
edes sinkala 2018-09-15 22:58:53

duu kwa upande wangu samata apambane zaidi akacheze ligi yoyote atakayoona ni bora

Avatar
hamisi msafiri 2018-10-09 22:42:11

poa sana lakini fanya mpango uingie leicester ili ufurahishe wananchi wetu.

Avatar
mkude simba shimon 2019-06-18 18:04:11

Mimi maoni yangu nafurahisana kuona mbongo


mwenzangu kwenda ligi yawabe huko kwakina wnyama twataka tuone uwezo wake

Avatar
vicent mahundu 2019-07-11 00:08:06

Mimi namuomba aendee England ili atufuraishe wabongo wezake mana Kule ndiko kwenye ligi ambaro linafuatiliwa sana duniani

Avatar
vicent mahundu 2019-07-11 00:08:27

Mimi namuomba aendee England ili atufuraishe wabongo wezake mana Kule ndiko kwenye ligi ambaro linafuatiliwa sana duniani

Avatar
vicent mahundu 2019-07-11 00:10:00

England aendee