banner68
banner58

Baada ya zoezi la kurejesha fomu kukamilika, uongozi Simba wataja kinachofuata

Baada ya zoezi la kurejesha fomu kukamilika, uongozi Simba wataja kinachofuata

16 September 2018 Sunday 07:40
Baada ya zoezi la kurejesha fomu kukamilika, uongozi Simba wataja kinachofuata

Uongozi wa Simba umetangaza rasmi jana kukamilisha zoezi la urejeshwaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya klabu hiyo.

Taarifa kutoka Simba imesema tayari wanachama wote waliokuwa wamechukua fomu wamesharudisha ili kupisha hatua nyingine inayofuata.

Uongozi huo umeeleza kuwa zoezi linalofuata hivi sasa ni mchakato wa usaili wa fomu hizo ambao utafanyika kesho Jumatatu.

Zoezi hilo litafanyika kabla ya kuelekea kampeni ambapo kila mwanachama ataruhusiwa kunadi sera zake kwa ajili ya kuwavutia watakaowapigia kura.

Ikumbukwe Simba itafanya uchaguzi wake mkuu Novemba 3 2018 ili kuwapata viongozi wengine watakaoongoza klabu hiyo kwa miaka minne ijayo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.