Bocco apiga mbili Simba yashinda 4-0 mechi ya kirafiki Afrika Kusini

Bocco apiga mbili Simba yashinda 4-0 mechi ya kirafiki Afrika Kusini

23 July 2019 Tuesday 13:59
Bocco apiga mbili Simba yashinda 4-0 mechi ya kirafiki Afrika Kusini

Rustenburg, Afrika Kusini
TIMU ya Simba SC leo imetoa onyo baada ya kushinda mabao 4-0 dhidi ya wenyeji,Orbret TVET  katika mchezo wa kirafiki wa mazoezi  katika uwanja wa Rustenburg, Afrika Kusini ambako imeweka kambi kujiandaa na msimu mpya. 

Nyota wa mchezo wa leo ni mshambuliaji, John Bocco  aliyefunga mabao mawili peke yake dhidi ya timu hiyo. Amefunga dakika ya 9 na 28.
 
Mabao mengine yamefungwa na Dilunga dakika  23 na Mbrazil, Da Silva kunako dakika 64 . Mechi hiyo ya kirafiki ilianza kupigwa majira ya saa 5 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki
 
Wakati huo huo afisa mtendaji mkuu wa klabu ya Simba, Crescentius Magori ameungana na timu hiyo na  alijumuika na wachezaji pamoja  na benchi la ufundi katika chakula cha usiku.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.