banner68
banner58

Bocco, Okwi, Kagere kuanza pamoja Simba ikiikabili Ndanda

Bocco, Okwi, Kagere kuanza pamoja Simba ikiikabili Ndanda

14 September 2018 Friday 18:24
Bocco, Okwi, Kagere kuanza pamoja Simba ikiikabili Ndanda

Kocha wa Simba, Patrick Aussems amepania kushinda kwa mabao mengi kesho kutokana na lengo lake kuanzisha kwa pamoja  washambuliaji wake watatu John Bocco, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere.

Mbinu ya kocha huyo kuendeleza rekodi ya ushindi dhidi ya Ndanda ilionekana katika mazoezi waliyokuwa wakifanya jioni hii kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Katika mazoezi hayo kocha Aussems amewagawa katika timu mbili tofauti na huenda kikosi kimoja ndio kikaanza kesho.

Timu ya kwanza ina wachezaji Aishi Manula, Shomary Kapombe, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Erasto Nyoni, Pascal Wawa, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mohammed Ibrahim, John Bocco, Emmanuel Okwi na Meddie Kagere.

Kikosi hiki ndio kinaweza kuwa kikosi cha kwanza kuelekea katika mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Ndanda.

Kikosi kingine kina Deogratious Munishi 'Dida', Adam Salamba Cleatus Chama, Said Ndemla, James Kotei, Poul Bukaba, Nicholas Gyan Rashid Juma na Marcel Kaheza.

Kikosi hiki kinaweza kuwa wale wachezaji wa akiba ambao watakuwa katika benchi dhidi ya Ndanda kesho.

Simba wanaingia katika mechi na Ndanda kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona huku wakiwa hawana rekodi ya kupoteza katika uwanja huo wala kufungwa na Ndanda tangu walivyopanda Ligi 2015.

Updated: 14.09.2018 18:32
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.