Bondia afariki baada ya kupigwa ulingoni

Bondia afariki baada ya kupigwa ulingoni

24 July 2019 Wednesday 08:52
Bondia afariki baada ya kupigwa  ulingoni

Moscow, Urusi 
Bondia raia wa Urusi Maxim Dadashev ameaga dunia baada ya pambano lake na Subriel Matias kumsababishia majeraha makubwa ya ubongo.

Dadashev mwenye miaka 28, alishindwa kutembea mwenyewe baada ya pambano hilo ambalo mkufunzi wake Buddy McGirt alilazimisha lisimamishwe katika raundi ya 11 baada ya bondia huyo kupokea kichapo kikali bila majibu.

Pambano hilo lilipigwa Ijumaa wiki iliyopita. Na punde tu baada ya pambano Dadashev alikimbizwa hospitali.

Madaktari waligundua kuwa damu ilikuwa ikimvuja kwenye ubongo na kufanyiwa upasuaji wa haraka, lakini akafikwa na umauti jana Jumanne.
Shirikisho la ndondi la Urusi limesema tayari uchunguzi umeshafuguliwa juu ya mkasa huo.

Katibu Mkuu wa shirikisho hilo, Umar Kremlev amedai kuwa kulikuwa na "aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu", na kuongeza kuwa: "Tumempoteza Maxim Dadashev. Ilikuwa ni nyota yetu inayochipua.

"Tutaiunga mkono familia yake, ikiwemo kifedha. Tutakamilisha uchunguzi wa kuangalia mazingira ya pambano, tunahitaji kujua ukweli wa kilichotokea.

"Hili linaweza kutokea kwenye mchezo wowote. Naamini kuna mapungufu ya kibinadamu yamechangia, kulikuwa na aina fulani ya uvunjwaji wa taratibu."

Dadashev ambaye alikuwa akifanya shughuli zake za masumbwi nchini Marekani alishinda mapambano yake yote 13 aliyoyacheza kabla.

Ijumaa alipambana na Matias kutoka Puerto Rico katika jimbo la Maryland ambapo alisukumiwa makonde mazito na kwa kasi kali.

Mkufunzi wa Dadashev, McGirt alieleza baada ya pambano kuwa "alishindwa kumshawishi" kukubali kushindwa, lakini akaamua kurusha taulo ulingoni baada ya kuona "akipigwa zaidi za zaidi kwa makonde ya wazi kadri pambano lilivyokuwa likiendelea."

BBC

Updated: 25.07.2019 13:35
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.