Bosi CAF aachiwa huru

Bosi CAF aachiwa huru

07 June 2019 Friday 17:40
Bosi CAF aachiwa huru

RAIS wa shirikisho la mpira Afrika(CAF) Ahmad Ahmad leo Juni 7, 2019 ameachiwa huru na mamlaka za kipolisi nchini Ufaransa.
 
Baada ya mahojiano hajakutwa na hatia wala kesi ya kujibu. 

Jana Juni 6, 2019 Shirikisho la soka duniani FIFA, lilithibitisha kukamatwa kwa rais  huyo ambaye alikuwa amehudhuria mkutano mkuu wa FIFA, jijini Paris Ufaranasa.

Taarifa ya FIFA ilisema Ahmad raia wa Madagascar, alikamatwa na kuhojiwa kuhusu madai mbalimbali kama rais wa CAF.

Hata hivyo, FIFA imesema kwa sasa haiwezi kutoa maelezo zaidi kuhusu kilichosababisha makamu huyo wa rais wa shirikisho hilo la soka duniani kutiwa mbaroni.

FIFA pia imewaomba maafisa wa uchunguzi nchini Ufaransa kuwapa taarifa zozote walizonazo, zinazoweza kuwasaidia katika Kamati yake ya ambazo zinaweza kuzisaidia katika Kamati yake ya maadili.

Ahmad alichaguliwa kuwa rais wa CAF mwaka 2017 baada ya kumshinda rais wa zamani Issa Hayatou raia wa Cameroon aliyekuwa ameongoza soka barani Afrika tangu mwaka 1988.

Taarifa zinadai Ahmad alituhumiwa kwa  rushwa na matumizi mabaya ya ofisi yake, akihusishwa na kampuni ya Puma.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.