Brazil wafanya mazoezi makali juani

Brazil wafanya mazoezi makali juani

27 May 2019 Monday 15:38
Brazil wafanya mazoezi makali juani

WACHEZAJI wa Brazil wamefanya mazoezi yao juani katika maandalizi mashindano ya Copa America yatakayofanyika Juni.


Nyota wa Brazil, Neymar na wenzake walionekana wanafurahi mazoezi na mazingira ya jua katika kambi yao iliyopo Granja Comary.


Kikosi cha kocha Tite kimesheheni wachezaji kama Gabriel Jesus na Fernandinho pamoja na Neymar, walionekana wakiwa na morali ya hali ya juu wakati mazoezi yao juani.


Brazil itafungua kampeni za Copa America hapo Juni 15 kwa kucheza dhidi ya Bolivia kabla ya kuivaa Venezuela na kumaliza na Peru katika mechi za hatua ya makundi.


Brazil inasaka kutwaa taji la kwanza la Copa Amerika tangu mwaka 2007, iliponyakuwa ubingwa huo kwa kuifunga Argentina 3-0 katika fainali zilizofanyika Venezuela

Updated: 28.05.2019 09:47
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.