Brazil yatwaa ubingwa Copa America

Brazil yatwaa ubingwa Copa America

08 July 2019 Monday 09:13
Brazil yatwaa ubingwa Copa America

TIMU ya  soka ya Brazil imefanikiwa kuchukua ubingwa wa Copa America baada ya kuichabanga timu ya Peru kwa goli 3-1. Ni ubingwa wa kwanza wa Brazil ndani ya miaka 12 ya mashindano hayo 

Mshambualiaji wa Man City, Mbrazil, Gabriel Jesus alifunga goli moja na kusaidia upatikanaji wa goli lingine

Paolo Guerrero wa Peru alirejesha matumaini kufuatia goli lake la kusawazisha.

Kunako dakika ya 15 kipindi cha kwanza, Mbrazil Sousa Soares aliiandikia timu yake goli la kuongoza baada ya kupata pasi mujaraba kutoka kwa Jesus. 

Lakini dakika ya 44, Mperu Guerrero aliisawazishia timu yake lakini  kunako dakika tatu za nyongeza Jesus aliiongeza goli la pili.

Hata hivyo dakika ya 70 kipindi cha pili, Jesus alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada ya kupata kadi ya pili ya njano.

Kalamu ya magoli ya Brazil ilihitimishwa kunako dakika 90  kwa njia ya penati  na mchezaji  Richarlison

Updated: 08.07.2019 10:20
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.