CAF yaishushia rungu Guinea U 17

"Guinea imepata pigo hilo baada ya kugundulika kuwa iliwachezesha wacheza wawili Aboubacar Konte na Ahmed Tidiane Keita "

CAF yaishushia rungu Guinea U 17

"Guinea imepata pigo hilo baada ya kugundulika kuwa iliwachezesha wacheza wawili Aboubacar Konte na Ahmed Tidiane Keita "

19 May 2019 Sunday 10:23
CAF yaishushia rungu Guinea U 17

SHIRIKISHO la Mpira wa miguu barani Afrika (CAF) kupitia baraza lake la nidhamu limeifungia Timu ya Taifa ya Guniea  chini ya umri wa miaka 17  kushiriki mashindano yajayo ya Kombe la Afrika na Dunia kutokana na udanganyifu wa  umri wa wachezaji wao walioshiriki mashindano ya Kombe la  Afrika  kwa vijana wa umri huo yaliyomalizika hapa jijini Dar es Salaam April 2019.

Guinea imepata pigo hilo baada ya kugundulika kuwa  iliwachezesha wacheza wawili  Aboubacar Konte na Ahmed Tidiane Keita wakati wa mechi baina yao na Senegal na Guinea kuibuka na ushindi wa mabao 2 - 1

Baraza la nidhamu la CAF lilitangaza  uamuzi wake mwishoni mwa wiki, Mara baada ya  kumalizika kwa mkutano wake ulifanyika Makao Makuu ya CAF, Cairo Misri kusikiliza Malalamiko ya Senegal. 

CAF imebaini vyeti vya kuzaliwa wachezaji hao vilionesha kuwa walizaliwa 2002 wakati vielelezo vyao vya awali  kwenye mashindano ya kombe la Dunia chini ya umri wa miaka 17 yaliyofanyika  nchini Japan 2017 vilionesha kuwa walizaliwa 2001

Tanzania ambayo ili kuwa mwenyeji wa  mashindano hayo na kushiriki katika fainali hiyo kwa mara ya kwanza ilitolewa akatika hatua za awali baada ya kupoteza michezo yake yote katika hatua za Makundi na ubingwa kwa Afrika kwa vijana hao kutwaliwa na timu ya Taifa ya Cameroon kwa mara ya pili mfululizo.

Updated: 19.05.2019 13:42
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.