David Beckam azua balaa Old Trafford

David Beckam azua balaa Old Trafford

27 May 2019 Monday 15:19
David Beckam  azua balaa Old Trafford

KIWANGIO alichokionyesha, David Beckham katika mchezo wa kirafiki wa wachezaji wa zamani ‘maveterani’ wa Manchester United na Bayern Munich kimezua mijadala kwenye mitandao ya kijamii.


Mashabiki wa Manchester United, wameibukia huko na kuanza kusema kwa viwango ambavyo vimeonyesha na mawinga wao msimu huu basi Beckham anauwezo wa kucheza kwenye kikosi chao cha kwanza.


Beckham alikuwa miongoni mwa mastaa wa  Manchester United walioungana jana usiku kwenye uwanja wa Old Trafford na kucheza mchezo huo wa kirafiki.


Maveterani wa Manchester United ambao waliifunga Bayern Munich mabao 5-0, walikuwa wakinolewa Sir Alex Ferguson.


Mashabiki wa Manchester United kwenye mitandao ya kijamii wanadai kuwa Beckham anaweza kuwaongezea nguvu upande wa winga ya kilia.


Akiwa kijana katika ubora wake kwenye kikosi chenyewe cha Manchester United, Beckham  aliichezea timu hiyo michezo 394 ambapo aliifungia mabao 85 na kutoa usaidizi kwenye mabao 152.


Beckham alishinda mataji sita ya Ligi Kuu England kwenye miaka ya 1995/96, 1996/97, 1998/99, 1999/00, 2000/01 na 2002/03 huku mawili yakiwa ya FA, 1995/96 na 1998/99, Ligi ya Mabingwa mara moja, 1998/99.

Updated: 27.05.2019 16:44
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.