banner68
banner58

Dawa ya Okwi yachemka Mtibwa Sugar

Dawa ya Okwi yachemka Mtibwa Sugar

11 August 2018 Saturday 20:26
Dawa ya Okwi yachemka Mtibwa Sugar

Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila ametamka anaisubiri kwa hamu Simba katika mechi yao ya Ngao ya Jamii kwani tayari anayo dawa ya kudhibiti nyota wake wakiongozwa na Emmanuel Okwi.

Simba na Mtibwa zitavaana Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza na Katwila alisema anajua sifa wanazomwagiwa kina Okwi na wenzake akiwamo Meddie Kagere na Adam Salamba, ila amewaandaliwa wa kuwadhibiti.

Alisema Hassan isihaka, Casian Ponela na Dickson Daud wamepewa kazi maalumu ya kuwazima nyota hao wa Simba na kazi itakuwapo Kirumba.

"Maandalizi tunayofanya ni makubwa kuona tunawafunga Simba nyinyi mnapenda kuwasifia sana, sisi tutafanya kwa vitendo," alitamba Katwila.

"Pamoja na ubora wao kwenye kikosi changu nina wachezaji imara watakaweza kupambana nao. Nina Isihaka, Ponela, Dickson Daud na wengine, nitaangalia watakavyokuja," alisema Katwila.

Alisema, kwa sasa wanaendelea na mazoezi na kucheza mechi za kirafiki ambapo jana Jumamosi walitarajia kukipiga na KMC kwenye Uwanja wa Bandari, jijini Dar.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.