Du David De Gea yaanza kumkuta!

Du David De Gea yaanza kumkuta!

12 June 2019 Wednesday 07:35
Du David De Gea yaanza kumkuta!

Kipa wa  Manchester United,  David De Gea ameendelea kusota kwa kutopata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza  cha  timu yake ya taifa ya Hispania katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Euro dhidi ya Sweden.


De Gea hajapata nafasi ya kuanza kwenye michezo mitatu iliyopita ya Hispania na badala yake amekuwa akitumika kipa wa Chelsea, Kepa Arrizabalaga.


Kutopata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza cha Hispania kunatajwa kuchangiwa na makosa mengi binafsi aliyokuwa akifanya katika michezo ya mwishoni mwa msimu akiwa na klabu yake ya Manchester United.


Kocha msaidizi wa Hispania, Roberto Moreno alisema ukiangalia viwango vya makipa watatu walionao kwenye kikosi chao ni Kepa ambaye amekuwa na uwiano mzuri wa kutoruhusu mabao.


“Tunamakipa watatu ambao wote ni bora, lakini Kepa amecheza fainali ya Europa Ligi na kufanya vizuri, tukaona tuchukulie hilo kama faida kwenye kikosi chetu na sio vinginevyo,” alisema.


Kepa  katika msimu uliomalizika  wa  2018-19  ndiye kipa wa Hispania aliyemaliza msimu kwa mafanikio ambapo walitwaa ubingwa wa Europa Ligi kwa kuwa mchezaji muhimu kwenye mchezo wa fainali Baku dhidi ya Arsenal.


Kinda huyo amekuwa na wakati mzuri msimu huu hata upande wa Ligi Kuu England pamoja na kuwa huu ni msimu wake wa kwanza ameonyesha kiwango bora kwenye michezo mfululizo tofauti na De Gea.

Updated: 12.06.2019 14:24
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.