Emmanuel Amunike aishtaki TFF kwa Fifa

Emmanuel Amunike aishtaki TFF kwa Fifa

12 September 2019 Thursday 10:55
Emmanuel Amunike aishtaki TFF kwa Fifa

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

ALIYEKUWA kocha wa timu ya soka nchini Tanzania Emmanuel Amunike amelishtaki shirikisho la soka la Tanzania (TFF) kwa shirikisho la mchezo huo duniani (FiFa) akilalamikia kutolipwa haki yake.

Kupitia mtandao wa Complete Sport.com na Punching.com , Kocha huyo raia wa Nigeria ameamua kuwasilisha malalamishi hayo kwa Fifa ili kutafuta haki yake.

Amunike alitimuliwa na TFF mara baada ya Taifa Stars kupata matokeo duni katika kombe la mataifa ya Afrika .

''Nimewasiliana na Fifa juu ya hilo jambo . Sio Swala la kupiga kelele , lakini nina imani watalitazama na kuamua iwapo ni sahihi mtu kutolipwa baada ya kufanya kazi'', Amunike amenukunuliwa katika mtandao huo.

Kocha huyo ambaye mkataba wake ulivunjwa mwezi Julai mwaka huu amerejea nchini Hispania ambako kwa sasa ndipo yalipo makazi yake ya kudumu .

Kwa mujibu wa TFF waliafikia uamuzi huo wa kuvunja mkataba na kocha mchezaji huyo wa zamani wa Nigeria baada ya taifa Stars kuandikisha matokeo mabaya katika fainali ya Afcon 2019 nchini Misri zilizofanyika kati ya Juni 21 hadi Julai 19.

Katika fainali hizo taifa Stars ilishika mkia kwenye kundi C lililokuwa na Senegal, Kenya, na Algeria baada ya kupoteza mechi zote tatu

Kushindwa kwao na majirani zao kenya ndio kulikohuzunisha wengi kwa kuwa walipoteza uongozi waliokuwa nao wa 2-0 kufikia kipindi cha mapumziko.

Na kufuatia matokeo hayo Amunike alisema kwamba timu hiyo ilihitaji uzoefu wa mashindano makubwa na kwamba wachezaji walihitaji kushiriki katika ligi zenye ushindani mkubwa ili kuweza kuimarika.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 47 ambaye hakuwa na kazi tangu alipoondoka klabu ya Sudan ya A; Khartoum mnamo mwezi Machi aliingia mkataba wa miaka miwili na TFF akichukua nafasi ya kocha Saulm Mayanga.

Amunike alishinda kombe la Afrika akiichezea Super Eagles ya Nigeria 1994 na mshindi wa dhahabu ya Olimpiki miaka miwili baadaye.

Katika kipindi chake cha mchezo aliichezea, SC Zamalek, Sporting lisbon, na Barcelona ijapokuwa majeraha yalimzuia kufikia ndoto yake mjini Catalonia.

Winga huyo wa zamani alianza ukufunzi na timu ya Nigeria isiozidi wachezaji wa miaka 17 2014 na kushinda kombe la dunia la makinda hao mwaka mmoja baadaye.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.