Etienne Ndayiragijje kocha mpya Taifa Stars

Etienne Ndayiragijje kocha mpya Taifa Stars

11 July 2019 Thursday 21:43
Etienne Ndayiragijje kocha mpya Taifa Stars

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
SHIRIKISHO la soka nchini (TFF) limemteua Etienne Ndayiragijje  kuwa kaimu kocha wa Taifa Stars kwa ajili ya mechi za kuwania tiketi ya Fainali za Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN) mwakani nchini Cameroon.

Taarifa ya TFF ya  leo  Julai 11, 2019 inaeleza uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha dharula cha Kamati ya Utendaji ya bodi hiyo ya soka nchini kilichofanyika leo.

Taarifa hiyo inaeleza Etienne ambaye ni kocha wa klabu ya Azam FC ya Dar es Salaam, amewapendekeza kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, Suleiman Matola kuwa wasaidizi wake.

Taifa Stars watakuwa wenyeji wa Harambee Stars Julai 27, 2019 katika mchezo wa kwanza raundi ya kwanza ya mchujo wa kuwania fainali za CHAN 2020, michuano inayohusisha wachezaji wanaocheza ligi za ndani pekee kabla ya timu hizo kurudiana Agosti 2 mjini Nairobi.

Uteuzi huo unakuja baada ya kufukuzwa kwa kocha Mnigeria, Emmanuel Amunike kufuatia Taifa Stars kupoteza mechi zote tatu za Kundi C kwenye Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2019 na taarifa ya TFF imesema uteuzi huo umezingatia programu maalumu ya kuendeleza makocha wazawa. 

Baada ya kufungwa 2-0 na Senegal, 3-2 na Kenya na 3-0 na Algeria, Taifa Stars iliondoka Misri bila hata pointi moja, ikishika mkia kwenye Kundi C, nyuma ya jirani zao, Kenya waliovuna pointi tatu, huku Senegal iliyomaliza na pointi sita katika nafasi ya pili ikiungana na Algeria iliyokusanya pointi tisa kwenda hatua ya 16 Bora.

Updated: 11.07.2019 21:51
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.