Ettiene Ndayiragije aaga KMC

Ettiene Ndayiragije aaga KMC

07 June 2019 Friday 17:09
Ettiene Ndayiragije aaga KMC

Na Oliver Albert, Dar es Salaam.
TIMU ya Soka ya KMC inasaka kocha mpya ili kuziba nafasi ya Ettiene Ndayiragije  ambaye inadaiwa anatimkia Azam FC.


Ndayiragije raia wa Burundi aliiongoza KMC kumaliza Ligi Kuu Bara  katika nafasi ya nne msimu uliopita hivyo pia kuiwezesha kupata nafasi ya kushiriki kwa mara ya kwanza mashindano ya kimataifa. 


Tanzania imepata nafasi ya kuingiza timu nne kwenye mashindano ya kimataifa msimu huu (mbili Simba na Yanga zikitarajia kucheza Ligi ya Mabingwa Afrika na nyingine mbili Azam na KMC zitacheza Kombe la Shirikisho Afrika.)


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya KMC FC,Mstahiki Meya Benjamin Sitta imesema licha ya uongozi wa klabu hiyo kutaka kumuongezea mkataba Ndayiragije lakini kocha huyo alifikia uamuzi wa kutoongeza mkataba kwa madai ya kutafuta changamoto sehemu nyingine.


Taarifa hiyo ilisema wanamshukuru Ndayiragije kwa mchango mkubwa alioutoa akiwa na KMC na wanamtakia mafanikio huko aendako.
Alisema KMC iko katika mchakato wa kutafuta kocha mwingine.


Kabla ya kujiunga na KMC,Ndayiragije alikuwa akiifundisha Mbao FC ya Mwanza na aliiwezesha kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho (FA) msimu wa 2016/2017  na kupoteza dhidi ya Simba kwa mabao 2-1.


Ndayiragije  amejizolea umaarufu mkubwa  wa kuibua vipaji ambavyo vimekuwa tishio kwenye Ligi Kuu.


Azam inatajwa kuwa tayari imemalizana na kocha huyo.

Updated: 11.06.2019 19:53
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.