banner68
banner58

Francis Kahata presha tupu Yanga

Francis Kahata presha tupu Yanga

14 July 2018 Saturday 11:05
Francis Kahata presha tupu Yanga

KAMA unadhani Yanga haiko vizuri basi ni wewe tu kwani kiungo fundi wa Gor Mahia, Francis Kahata, ameanza kupagawa akihofia mziki wa vijana wa Jangwani.

Yanga itaondoka nchini mapema wiki ijayo kuifuata Gor Mahia kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi. Gor jana ilikuwa inamalizia Kombe la Kagame kwa mechi yake ya kusaka mshindi wa tatu.

Sasa kuelekea mechi ya shirikisho, Kahata ameonyesha wasiwasi kuikabili Yanga akisema Gor wamekuwa na ratiba ngumu hivyo, Yanga inaweza kuwapa wakati mgumu kwelikweli.

Akizungumza na gazeti la michezo la Mwanaspoti, Kahata alisema ratiba imekuwa mbaya zaidi kwa upande wao kwani baada ya kumalizana na michuano ya Kagame sasa wanakwenda kwenye Shirikisho ambako kuna vigogo wakali.

“Kiukweli hata kufika hatua hii tumejitahidi sana kwa sababu hatukupata muda wa kupumzika, tulitoka katika mechi ya Ligi Kuu Kenya na kuja huku ambako tumecheza mechi mfululizo. Licha ya kuchoka lakini bado tumeonyesha kitu kwenye mashindano haya,” alisema.

Kahata aliongeza kuwa akiangalia ratiba ya mbele yao ndio anaumia zaidi kwa sababu wana mechi nyingine mfululizo ambazo zote ni muhimu.

“Tuna mechi ya ligi kabla ya Yanga ambazo zote tunahitaji kushinda, pia tuna mechi dhidi ya watani wetu AFC Leopards,” alisema.

Gor Mahia itaikaribisha Yanga Julai 17 kule jijini Nairobi, Kenya.

Mwanaspoti

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.