banner68
banner58

Habari Njema: Samatta kuelekea League 1 nchini Ufaransa

Habari Njema: Samatta kuelekea League 1 nchini Ufaransa

25 June 2018 Monday 09:03
Habari Njema: Samatta kuelekea League 1 nchini Ufaransa

Na Amini Nyaungo

Baada ya kushuhudia rafiki yake mkubwa Mbwana Samatta, Omar Colley ambaye alikuwa naye KRC Genk ya Ubelgiji,akitimkia Sampdoria ya Italia zamu ya nahodha wa Tanzania imekaribia kutua Ufaransa.

Unakumbuka mwezi Oktoba 2017 Samatta alisema kuwa ataweza kuondoka KRC Genk na kuelekea ligi tano kubwa sasa uongozi unaomsimamia inataka kumpeleka Olympique De Marseille.

Samatta anasimamiwa na Sportback ambayo pia inasimamia baadhi ya wachezaji wengine kutoka bara la Afrika, Ufaransa na Uswizi ni moja ya sehemu ambayo kampuni hiyo inafanya biashara kwa karibu sana.

Ndani ya kampuni hiyo  mchezaji ghali zaidi ni Samatta ambaye katika mtandao wa ‘Transfer Market’ inasemekana  anathamani ya bilioni 8 za kitanzania.

Omar Colley ambaye nasimamiwa na CLS Mundial imefanya jitihada kubwa hadi mchezaji huyo kutua Italia na msimu huu unaoanza Augusti atakuwa katika kikosi cha Sampdoria.

Updated: 25.06.2018 10:27
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Masunga 2018-07-02 15:34:35

Ongela Samata

Avatar
martine.m 2018-07-08 14:29:14

kila raheli samatta huko uendapo

Avatar
martine.m 2018-07-08 14:31:41

kila raheli samatta huko uendapo

Avatar
Daud M Mogoyo 2018-07-10 17:08:02

Je,mnayoyaongea ni kweli au ni uvumi na visanga? Samatta kwenda Ufaransa

Avatar
mohamedi kilimo 2018-07-11 23:26:45

hongera Samara kwa kazi nzuri unayo ifanya pia ni mfano kwa nchi yetu

Avatar
Pius john 2018-07-22 14:10:31

Tanzania juu, Samata juu.

Avatar
omaly kilunda 2018-10-22 19:06:08

pamoja xana kijana

Avatar
samsonh 2018-11-02 21:10:25

ongera sana samatta kazi yako na dhaman yako inaonekana pamoja sana