Habari za ujali: Yanga wahaha kuwabakisha wachezaji wake, Simba kama Real Madrid, Kamusoko kuoga pesa za Azam

Tayari nyota wawili wa Yanga wanahusishwa na klabu za Simba na Azam

Habari za ujali: Yanga wahaha kuwabakisha wachezaji wake, Simba kama Real Madrid, Kamusoko kuoga pesa za Azam

Tayari nyota wawili wa Yanga wanahusishwa na klabu za Simba na Azam

30 May 2018 Wednesday 12:51
Habari za ujali: Yanga wahaha kuwabakisha wachezaji wake, Simba kama Real Madrid, Kamusoko kuoga pesa za Azam

Na Amini Nyaungo

Wakati ikiwa siku ya mbili tangu dirisha la usajili lifunguliwe, mabingwa wapya wa ligi kuu Tanzania Bara Simba wanaonekana wako vizuri kutokana na kuwa na fedha za kutosha katika usajili.

Msemaji mkuu wa timu hiyo Haji Manara amesema kuwa anataka kulipa kisasi japo hajasema kisasi hicho ni dhidi ya timu gani, japokuwa ni dhahiri kwamba kinaelekezwa kwa Yanga kwani tayari tetesi za nyota wawili wa timu hiyo wanahusishwa na kujiunga na wafalme wapya Simba.

Yanga

Klabu ya Yanga inahaha kuhakikisha kwamba wachezaji wake nyota ambao tayari mikataba yao inaelekea ukingoni wanaendelea kubaki ndani ya kikosi cha timu hiyo, huku katibu mkuu akithibitisha kuwa timu hiyo bado inaukata wa fedha.

Yanga inaelekea nchini Kenya katika michuano ya SportsPesa Super Cup, huku ikiwa haina uhakika kama itaweza kuwa na wachezaji wake wawili nyota, kiungo Papy Tshishimbi na beki wa kati Kelvin Yondani ambao wanahusishwa na kujiunga na Simba.

Licha ya viongozi wa Yanga kukana juu ya uwezekano wa wachezaji hao kuondoka, lakini bado kuna wingu zito limetanda katika anga za mitaa ya Twiga na Jangwani.

Simba

Baada ya kutamba kuwanasa wachezaji wawili Adam Salamba na Marcel Kaheza sasa wamehamia kwa kiungo wa Yanga Tshishimbi na beki Kelvin Yondani.

Simba ina fedha kwa ajili ya kufanya usajili wa wachezaji ambao wanaweza kuisaidia katika kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa mwakani, hivyo inafanya lolote linalowezekana kuhakikisha kuwa wanaunda kukosi kuzuri ambacho kitakuwa na ushindani na kufanya vizuri Afrika na katika mashindano ya ndani.

Singida United

Uongozi wa Singida United unahusishwa na kumsajili nyota wa JKU ya Zanzibar Feisal Salum, huku uongozi wa JKU ukisema mchezaji huyo ana mkataba wa miaka 5, hivyo kama wanahitaji huduma ya mchezaji huyo, Singida United hawana budi kufuata utaratibu sahihi.

Azam FC

Timu ya Azam wanaendelea kusajili kimya kimya ikiwa tayari wamenasa saini za wachezaji wawili Donald Ngoma na Tafadzwa Kutinyu, huku wakitaka kuibomoa Yanga kwa kupata huduma ya Thabani Kamusoko.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.