banner58

Habari za usajili: Manara ataka kuilipa kisasi Yanga

Habari za usajili: Manara ataka kuilipa kisasi Yanga

29 May 2018 Tuesday 11:33
Habari za usajili: Manara ataka kuilipa kisasi Yanga

Na Amini Nyaungo

Tangu dirisha la Ligi kuu Tanzania Bara lifunguliwe vilabu vya Simba na Azam vimekuwa vikifanya kweli katika kuboresha vikosi vyao kwa ajili ya msimu ujao wa ligi na michuano ya kimataifa.

Msemaji mkuu wa Simba Haji Manara amesema watalipa kisasi kwa wote waliowahi kuwanyanyasa kipindi cha nyuma.

“Tunaenda Kenya na kuna habari kubwa tunaenda nayo, mie nasema tutalipa yote waliowahi kutufanyia,” amesema Manara.

Manara hakusema timu gani anataka kuilipia kisasi lakini ni dhahiri kuwa alikuwa akizungumza kuhusu watani wake Yanga ambayo kipindi hiki ina matatizo ya kifedha.

Simba

Mabingwa wa ligi kuu Tanzania Bara 2017-2018 tayari wamefanya biashara asubuhi mara baada ya kuwasajili Adam Salamba kutoka Lipuli FC ta Iringa pamoja na Marcel Kaheza kutoka Majimaji ya Songea wote wakicheza nafasi ya ushambuliaji.

Azam

Azam wamemsajili mshambuliaji wa Yanga Donald Ngoma na Tafadzwa Kutinyu, huku wakiripotiwa kuhitaji huduma za winga Deus Kaseke wa Singida United pamoja na Thabani Kamusoko wa Yanga.

Yanga

Mabingwa wa zamani ligi kuu bara bado hawaelewi nini wafanye maana hakuna kinachoendelea hadi sasa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.