Habari za usajili Tanzania Bara: Simba na Yanga kupigana vikumbo

Simba na Yanga wanahitaji wachezaji baada ya kuwa na makocha wapya ambao walirithi wachezaji walioachwa na watangulizi wao

Habari za usajili Tanzania Bara: Simba na Yanga kupigana vikumbo

Simba na Yanga wanahitaji wachezaji baada ya kuwa na makocha wapya ambao walirithi wachezaji walioachwa na watangulizi wao

23 May 2018 Wednesday 12:31
Habari za usajili Tanzania Bara: Simba na Yanga kupigana vikumbo

Na Amini Nyaungo

Wakati Ligi Kuu Tanzania bara inaisha siku ya jumatatu kuna idadi kubwa ya makocha na wachezaji wataweza kuondoka na kuelekea katika vilabu vingine.

Simba na Yanga wanahitaji wachezaji baada ya kuwa na makocha wapya ambao walirithi wachezaji walioachwa na watangulizi wao, na watahitaji kuwa na wachezaji ambao wataendana na mfumo wanaotaka kuutumia.

Simba

Mabingwa wa soka Tanzania Bara klabu ya Simba imeingia miguu miwili kwa mchezaji wa Lipuli, Adam Salamba ambapo Yanga walishindwa kumpata baada ya uongozi kuweka kauzibe.

Simba wako katika mchakato wa kuimarisha kikosi chao kwa kuhitaji nyota wengi wazuri ili kufanya vizuri katika michuano ya klabu bingwa ya Afrika.

Yanga

Klabu ya Yanga imemleta mchezaji kutoka Nigeria ambaye bado jina lake halijafahamika kwa ajili ya majaribio katika harakati za michuano ya kombe la shirikisho pamoja na michuano ya ndani.

Mchezaji huyo atakuja kuziba nafasi ya Donald Ngoma ambaye inasemekana ameachwa na timu hiyo.

Azam

Azam FC wako mbioni kumtangaza kocha mkuu Hans Van Pluijm ambaye atachukua mikobo ya Aristica Ciaoba.

Huku uongozi wa timu hiyo ikionekana kufanya mambo yake kimya kimya, habari za ndani kutoka katika timu hiyo zinasema wako tayari kutumia pesa kwa ajiri ya kuimarisha kikosi chao.

Singida United

Timu hiyo baada ya kuagana na aliyekuwa kocha mkuu Mdachi Hans Van Pluijm inasemekana ataenda Azam FC, inasemekana wapo katika mazungunzo ya kuhitaji saini ya aliyekuwa kocha wa Mbao FC Etienne Ndayiragije huku mtendaji mkuu wa Singida United Festo Sanga akithibitisha kuongea na kocha huyo.

Kinondoni Municipal Council (KMC)

Timu hiyo ambayo imepanda daraja msimu huu hadi Ligi Kuu Tanzania Bara, inahitaji saini ya kocha Etienne Ndayiragije ambaye pia anahitajika Singida United.

Wakati huo huo bado haijafahamika hatma ya kocha aliyepandisha timu hiyo Fredy Felix Minziro kama wataendelea naye au wataachana naye, huku ikisemekana ataachwa.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
ANWALY 2018-08-13 09:11:47

0625095189