Haji Manara atoa ya moyoni juu ya mechi ya Yanga na Stand United

Haji Manara atoa ya moyoni juu ya mechi ya Yanga na Stand United

17 September 2018 Monday 08:04
Haji Manara atoa ya moyoni juu ya mechi ya Yanga na Stand United

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameibuka na kuwapiga dongo watani zake wa jadi kuwa mpira waliocheza dhidi ya Stand United jana walitamani mechi iishe mapema.

Manara amefunguka na kueleza kuwa Yanga haikucheza mpira wa kifundi na badala yake walizidiwa kimbinu jambo ambalo lilisababisha wakoswe mabao kadhaa.

Ofisa Habari huyo mwenye maneno mengi zaidi, ameeleza kuwa Yanga waliona hali ngumu na kuanza kuomba mechi iishe haraka ili wasalie na matokeo yao ambapo walikuwa wanaongoza.

Mara baada ya Alex Kitenge kufunga bao la tatu, Manara aliamini kuwa Stand wangeweza kusawazisha na kuongeza mengine kutoka na watani zake walianza kuelemewa uwanjani.

Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Taifa jana, Yanga ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 4-3 huku kipa wake Mkongo Klaus Kinzi Kindoki akipewa lawama juu ya mabao aliyofungwa.
 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
january ful 2018-09-17 11:36:16

huyu alisema abadai hawezi kuwa msemaji wa yanga vipi mbona sasa analonga ya yanga,mbaya Zaidi bila malipo!!!!!

Avatar
Silaa 2018-09-18 09:55:30

Boya huyo

Avatar
Ding Veno 2018-10-31 10:34:41

Yao Yamewashnda