Haji Manara na Dismas Ten nani msemaji bora ligi kuu Tanzania Bara?

Haji Manara na Dismas Ten nani msemaji bora ligi kuu Tanzania Bara?

28 May 2018 Monday 11:27
Haji Manara na Dismas Ten nani msemaji bora ligi kuu Tanzania Bara?

Na Amini Nyaungo

Wakati leo ligi kuu Tanzania bara inafikia tamati leo, huku Yanga Simba na Azam zikiwa katika nafasi tatu za juu.

Mchezo wa Yanga na Azam ndio mkubwa wakigombania nafasi ya pili wakati Ndanda wakitaka kujinasua kushuka daraja huku Majimaji naye akitegemea amfunge Simba ili apite na abakie ligi kuu Bara.

Azania Post inaendelea na uchambuzi wa ligi kuu inayomalizika leo.

Baada ya kuona timu bora, mabeki bora wa pembeni na nani anafaa kuwa mchezaji bora, leo inakuletea orodha ya wasemaji wakuu watano waliofanya vizuri pamoja na changamoto zao.

Haji Manara

Huyu ndiye Msemaji mkuu wa klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam.

Manara ana mbwembe sana na ni mmoja ya watu wanaolifahamu vizuri soka la Tanzania.

Licha ya usemaji bado Manara ni mchambuzi mzuri wa soka kama ulikuwa hujui.

Kuna wakati huwa anapitiliza katika pale anapokuwa anaizungumzia Yanga ambao ndiyo watani wa jadi wa timu yake, lakini anaposimama kusema jambo huwa analifanya kwa 100%.

Ukweli ni kwamba, anaufahamu mzuri sana wa mpira wa miguu.

Kwa upande wa changamoto kubwa kwake ni povu tu hasa anapokuwa anatumia akaunti zake za mitandao ya kijamii, ambao huwezi kumsema sana kwakuwa kule akaunti binafsi.

Dismas Ten

Huyu ndiye Msemaji mkuu wa Yanga, ambaye hana maneno mengi kwa kuongea hamuwezi Manara, lakini moja ya wasemaji wanaotumia akili nyingi sana na amefanikiwa kuleta mabadiliko katika kikosi cha Yanga kwani ndiye aliyeleta wazo la Kalenda na Jarida la Yanga na muonekano mzuri wa ndani wa klabu hiyo.

Anaweza kuisaidia timu hiyo endapo watampa muda mrefu katika kuleta maendeleo na mabadiliko.

Jaffari Iddi Maganga

Huyu ni mmoja ya watu waliopata umaarufu sana hasa kwa kujenga hoja. Ameweza kuitetea Azam kwa namna anavyoweza, msemaji ambaye hana maneno mengi kwa timu nyingine, huwa anaongelea timu yake.

Masau Bwire

Maarufu kama ‘Mzee wa kupapasa’, huyu ndiye msemaji wa Ruvu Shooting. Ni mmoja ya watu walio na maneno ya kuchangamsha sana katika soka.

Kitaaluma ni mwalimu wa shule ya msingi hapa Dar es Salaam, maneno yake hayaudhi bali yamekuwa faraja pindi unapomfanyia mahojiano.

Msimu ujao tutaendelea kuwa nae katika ligi kuu Bara.

Thobis Kifaru

Msemaji wa mkuu wa Mtibwa Sugar na mmoja ya watu waliofanya kazi hiyo kwa zaidi ya miaka 15 na kwa mafanikio makubwa.

Kifaru naye anamaneno ya kuchekesha ambayo kama ilivyo kwa Masau Bwire imekuwa faraja hasa kwa mashabiki wa timu yake.

Katika tuzo ya msemaji bora wa msimu jukumu hilo tunakuachia wewe, pitia katika kurasa zetu za Instagram, Twitter na Facebook utuambie nani unamchagua.

Azania Post

Updated: 28.05.2018 11:34
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.