Harry Maguire aitaka Leicester imalizane na Man United

Harry Maguire aitaka Leicester imalizane na Man United

09 July 2019 Tuesday 15:28
Harry Maguire aitaka Leicester imalizane na Man United

London, Uingereza
BEKI wa kati, Muingereza  Harry Maguire amekubali yaishe na sasa ameitaka klabu yake ya Leicester City kukubali ofa ya Man United ya paundi milioni 70 ili imsajili 

Hatua yake hiyo ni kufuatia klabu ya Man City kujiondoa kuwania saini yake na sasa ameitaka klabu yake  ya Leicester kufikia muafa na Man United 

Leicester wanataka kulipwa paundi milioni 80 wakati Man United wameweka mezani ofa ya  paundi milioni 70

Mashetani wekundi  walianza kumwania  Harry Maguire miezi 12 iliyopita  chini ya kocha, Jose Mourinho .

Kiwango chake kimeendelea kuivutia Man United  na kocha wa timu hiyo Solskjaer.

Katika  harakati za kukiimarisha kikosi tayari Man United imeshamsajili beki, Aaron Wan-Bisska kutoka Crystal Palace  pamoja na winga kutoka Swansea, Daniel James.

Updated: 10.07.2019 06:01
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.