banner68
banner58

Haruna Niyonzima aibua jipya Simba

Kocha Patrick Aussems afunguka

Haruna Niyonzima aibua jipya Simba

Kocha Patrick Aussems afunguka

10 October 2018 Wednesday 19:54
Haruna Niyonzima aibua jipya Simba

Kocha Mbelgiji wa Simba, Patrick Aussems, amewapa shavu wachezaji wake wawili, Haruna Niyonzima na Juuko Murshid kwa kusema huu ni muda wa wachezaji hao kucheza zaidi.

Niyonzima na Juuko walikuwa sehemu ya kikosi cha Simba kilichocheza na African Lyon wikiendi iliyopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar, ambapo Niyonzima aliingia dakika ya 77 huku Juuko yeye akiishia kukaa benchi kama mchezaji wa akiba.

Kocha huyo amesema jijini kwamba kwa sasa anataka kufanya mabadiliko ya kikosi chake kwa kuhakikisha kila mchezaji anapata na­fasi ya kucheza ikiwemo wachezaji hao wawili ambao wameingia kwenye timu katika kipindi hiki.

“Nina wachezaji wengi hapa na kila mmoja anahitaji kucheza kwa ajili ya kuongeza uwezo wake, ni muda sasa wa ku­fanya mabadiliko katika kikosi kwa kumpa nafasi kila mmoja na ndiyo maana utaona hata Niyonzima amepata nafasi kwenye mechi yetu hii.

“Jambo am­balo ninataka kufanya ni kuo­na kila mmoja anacheza kwenye mechi zetu ili kuwa­fanya wawe na uwezo wa hali ya juu, la­kini sambamba na hilo ninahitaji pia kuboresha eneo langu la ushambuliaji,” alisema Mbelgiji huyo.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.