banner68
banner58

Hatimaye Masoud Djuma atupiwa virago Msimbazi

Hatimaye Masoud Djuma atupiwa virago Msimbazi

06 October 2018 Saturday 19:12
Hatimaye Masoud Djuma atupiwa virago Msimbazi

Yametimia! Baada ya vuta ni kuvute hatimaye kocha msaidizi wa Simba, Mrundi Masoud Djuma ametupiwa virago rasmini leo.

Mrundi Masoud ametimuliwa baada ya kukatisha mkataba wake na klabu hiyo kutokana na kutoelewana kwake na kocha mkuu Patrick Aussems.

Kumekuwa na mgogoro wa muda mrefu baina ya Masoud na bosi wake Mbelgiji Aussems na picha lilianza kuonekana wazi baada ya kuachwa jijini Dar es Salaam, timu hiyo ilipokwenda kucheza na Ndanda FC na kupewa jukumu la kufundisha timu ya vijana.

Kocha huyo wa zamani wa Rayon Sports maisha yake ndani ya Simba yalikuwa magumu tangu kuanza kwa msimu huu kutokana na kutoelewana kwake na Mbelgiji.

Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema wanajua Masoud ana mkataba wa miaka miwili na umebaki mwaka mmoja, lakini wapo tayari kumlipa fidia.

"Ana mkataba wa miaka miwili kama tutavunja mkataba wake basi atalipwa fidia zake zote anazostahili kulipwa," alisema Kaimu Rais.

Kuhusu kutokuwepo kwenye benchi jioni hii dhidi African Lyon alisema "Ni kweli hatakuwepo na kama atakuja basi atakaa jukwaani kama mashabiki wengine."

Mapema leo asubuhi Abdallah ‘Try Again’, alikiri kuwa kwa hali inavyoendelea baina ya makocha hao ni ngumu kwa Mrundi huyo kuendelea kubaki katika klabu hiyo.

"Tatizo la Masoud halijaanza leo, alianza kutoelewana na kocha Joseph Omog, akaja Pierre Lechantre na sasa Aussem, tumejaribu kuliweka sawa, lakini tunaona kadri muda unavyoendelea hali inakuwa ngumu.

"Lolote linaweza likatokea kuanzia sasa, hivyo siwezi kusema anabaki ama anaondoka bado ni mapema, ila ukweli ni kwamba hana maelewano mazuri na kocha mkuu na siyo kuwa na tatizo na viongozi wa Simba," alisema Try Again.

Djuma ambaye alichukuwa nafasi ya Jackson Mayanja alisaini mkataba wa miaka miwili ambapo uongozi umesema watamlipa fidia kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wao.

Habari kutoka ndani zinasema kwamba tayari uongozi umevunja mkataba na Djuna tangu jana Ijumaa

Katika mazoezi ya jana jioni Masoud Djuma alizua hofu kwa mashabiki baada ya kuchelewa kufikaa katika mazoezi hayo kwenye Uwanja wa Boko Veteran ikijiandaa na mchezo leo dhidi ya African Lyon.

Simba walianza mazoezi wakiwa na kocha mkuu Patrick Asseums huku Masoud akiwa haonekani.

Hata hivyo baada ya dakika 20, kocha huyo alifika uwanjani na moja kwa moja alimfuata mkuu wake Asseums na kumsalimia kisha akaenda kuangalia namna programu zingine zinavyoendelea.

Baada ya hapo alimchukua na kumsimamia kiungo Mzamiru Yassin ambaye alikuwa na programu maalum ya mazoezi pembezoni mwa uwanja.

Kukosekana kwa Masoud kwa dakika hizo kulizua maswali mengi kwa mashabiki wa Simba huku wakianza kuhofia kwamba tayari ameshaondoka.

Mwanaspoti

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
sosyshy 2018-10-08 19:20:53

Maamuzi magumu yanatijaSSC nguvumoja