Hemedi Morocco achukua kizizi cha Hans Van Pluijm

Singida United wamechukua uamuzi huo mara baada ya kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van Pluijm

Hemedi Morocco achukua kizizi cha Hans Van Pluijm

Singida United wamechukua uamuzi huo mara baada ya kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van Pluijm

02 June 2018 Saturday 18:02
Hemedi Morocco achukua kizizi cha Hans Van Pluijm

Na Amini Nyaungo

Aliyekuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibari Heroes, Hemed Morocco amejiunga na Singida United leo baada akitambishwa rasmi na Mtendaji Mkuu wa timu hiyo Festo Sanga.

Hii imekuja baada ya timu yake hiyo mpya kupoteza mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la shirikisho 'Azam Sports Federation Cup' uliofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha leo dhidi ya Mtibwa Sugar.

Singida United wamechukua uamuzi huo mara baada ya kuachana na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo Hans Van Pluijm ambaye ametimkia Azam.

Maneno ya awali ya kocha Morocco amesema kuwa anamtihani mkubwa wa kuifikisha mbali zaidi ya ilipofika sasa.

"Nina mtihani mkubwa sana kufika zaidi ya hapa ilipofika Singida, Hans amefanya kazi kubwa sana," amesema

Singida United imemaliza katika nafasi ya nne mbele ya Mtibwa Sugar katika msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara iliyomalizika hivi karibuni.

Licha ya kumtambulisha kocha huyo, bado timu hiyo imefanya usajili wa wachezaji watatu kuziba nafasi ambazo zimeonekana kuyumba msimu uliopita.

Azania Post

Updated: 03.06.2018 09:38
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.