banner68
banner58

Hiki ndicho kikosi kamili cha Simba 2018/2019

Yasheheni viungo mahiri na washambuliaji

Hiki ndicho kikosi kamili cha Simba 2018/2019

Yasheheni viungo mahiri na washambuliaji

27 July 2018 Friday 13:17
Hiki ndicho kikosi kamili cha Simba 2018/2019

Mabingwa wa tetezi wamefunga usajili wao huku wakiwa wamesajili mabeki 11 na viungo 11 katika orodha ya wachezaji wao 30 watakaowatumia katika msimu ujao.

Simba itakayowakilisha Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu ujao ina wachezaji nane wa kulipwa  kati ya nyota wake 30.

Safu ya ushambuliaji wa Simba inaundwa na wachezaji watano wawili wakiwa wa kigeni ambao ni Meddie Kagere kutoka Rwanda pamoja na Mganda Emmanuel Okwi mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara msimu uliopita.

Mbelgiji Patrick Aussems ni muumini wa soka la pasi nyingi kwa staili kama ya Pep Guardiola wa Man City, ambapo bao ni lazima zipigwe pasi zaidi ya 10.

Ameweka bayana kwamba, hataki soka la Kiingereza la pasi mbili wako golini wanafunga na kama wachezaji watashindwa kwenda na staili hiyo basi watapata tabu sana uwanjani.

“Kila mwalimu ana falsafa yake ya ufundishaji, timu yangu nataka imiliki mpira na kucheza soka la utulivu, sitaki wanapiga pasi mbili wako golini kwa wapinzani wanafunga bao, hapana hiyo staili yangu kabisa,” alisema Aussems.

Pia, alifichua kuwa anapenda kuwa kwenye timu ambayo wachezaji wake wanakuwa na furaha uwanjani kwa kuwa, itasaidia kuwapa morali wa kufanya vizuri uwanjani.

KIKOSI CHA SIMBA MSIMU WA 2018/19

MAKIPA:  Aishi Manula, Deogratius Munishi ‘Dida’, na Ally Salim

MABEKI: Shomali Kapombe, Asante Kwasi, Mohammed Hussein, Nickolas Gyan,  Paschal Wawa, Erasto Nyoni, James Kotei, Yusufu Mlipili, Paul Bukaba, Vicent Costa, Salim Mbonde.

 VIUNGO: Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Shiza Kichuya, Cletus Chama, Haruna Niyonzima, Hassan Dilunga, Mohammed Ibrahim,  Marcel Kaheza,  Abdul Hamis, Rashid Juma na Said Ndemla

 WASHAMBULIAJI: Emmanuel Okwi, John Bocco, Middie Kagere, Adam Salamba na Mohammed Rashid

BENCHI LA UFUNDI: Kocha Mkuu Patrick Aussems, Kocha Msaidizi Masoud Dhuma, Kocha wa Makipa,  Mwalami Mohammed, Kocha wa Viungo  Adel Zrane na Daktari wa timu Yassin Gembe .

Updated: 30.09.2018 12:49
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Michael simon 2018-07-27 21:48:48

mungu ibarik tmu yang ya simba sc.

Avatar
HALUNA MUSTAFA 2018-08-03 18:29:30

SIMBA WAKAZE SASA

Avatar
deus james 2018-07-29 10:38:33

simba bingwa 2018/2019

Avatar
Charles Silo 2018-07-28 21:41:32

Nimekipenda Kikosi, Nawakumbusha Kua Wasio Ipenda Simba Watapata Tabu Saana!

Avatar
ELIGIUS KOMBA,WA SONGEA LIZABON. 2018-11-03 06:28:18

SIMBA SC.SASA WANAPGA MPIRA MWINGI KAMA WA ULAYA AMINI MASHABIKI TUMEWAKUBALI,LEO TANZANIA PRISONS KAZ MNAYO.

Avatar
Innocent 2018-07-28 11:10:04

Naiamini simba yangu mwenyezi mungu waepushe majeruhi wachezaji wetu

Avatar
Saghad 2018-11-10 21:01:29

Simba nimoto yaan fire

Avatar
bene 2018-11-09 15:26:03

simba nimnyama