Himid Mao ajiunga na ENPPI ya Misri

Himid Mao ajiunga na ENPPI ya Misri

31 July 2019 Wednesday 11:09
Himid Mao ajiunga na ENPPI ya Misri

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam
MCHEZAJI kiungo, Himid Mao Mkami  amesaini mkataba wa kujiunga na klabu ya klabu ya ENPPI ya ligi kuu ya nchini  Misri.

Mao anajiunga na ENPPI baada ya klabu yake, Petrojet kushuka daraja kwenye ligi kuu ya Misri msimu uliopita. 

Akizungumza mara baada ya kutambulishwa katika klabu hiyo Mao amesema.“Nina furaha kujiunga na klabu yangu mpya, ENPPI na ninaelekeza nguvu zangu katika msimu mpya kwa ajili ya mafanikio zaidi”

Juni, 2018 Mao alijiunga na Petrojet  akitokea Azam FC, klabu iliyomuinua kisoka akianza kuichezea ngazi ya timu za vijana.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 aliyerithi kipaji cha baba, Mao Mkami ‘Ball Dancer’, kiungo wa zamani wa Pamba, Mtibwa Sugar na Moro United aliibukia akademi ya Elite mwaka 2005 kabla ya 2007 kujiunga na Azam.

Mao  alianza kuchezea timu za vijana za taifa Tanzania kuanzia umri chini ya miaka 15, U17, U20, U23 na hadi sasa ya wakubwa na tangu mwaka 2013 ameichezea Taifa Stars mechi 50 na kuifungia mabao mawili.

Updated: 03.08.2019 07:33
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.