banner68
banner58

Huu ndio mchoro wa Simba mpya ya `Mo`

Uwanja wa kisasa unakuja, ukiwa na mahitaji yote muhimu kwa wachezaji

Huu ndio mchoro wa Simba mpya ya `Mo`

Uwanja wa kisasa unakuja, ukiwa na mahitaji yote muhimu kwa wachezaji

20 June 2018 Wednesday 12:56
Huu ndio mchoro wa Simba mpya ya `Mo`

Na Amini Nyaungo

Baada ya kukubali uwekezaji ndani ya klabu ya Simba na kumpatia hisa 49% Mohamedi Dewji, muonekano wa Simba hiyo unakuja upya.

Simba sasa inauwezo wa kufanya chochote katika usajili huku ikiwa na mipango ambayo inatarajiwa kuwa ni mshangao mkubwa kwa wadau wa soka nchini.

Mchoro wa Simba mpya uko hivi

Klabu hiyo itakuwa na wachezaji wawili wenye viwango vya juu kila sehemu kuanzia kipa hadi namba kumi na moja.

Na aina ya mfumo huo wa kuwa na wachezaji wawili wenye viwango bora utafanya kila mmoja ajitume zaidi na hapo ndipo utaona timu ikicheza soka la hali ya juu.

Ule uwanja ambao ulikuwa unasubiriwa kwa hamu sasa wakati wake umefika na utaanza kufanyiwa ujenzi ndani ya mwaka huu na unategemewa kutumika katika msimu wa 2019/2020 kwa ajili ya michezo ya timu hiyo.

Katika sehemu ya uwanja kama alivyosema `Mo`, kutakuwa na hosteli kwa ajili ya wachezaji, Gym ya mazoezi pamoja na `canteen` kwa ajiri ya chakula cha wachezaji.

Aina ya uendeshaji utabadilika utaenda kisasa zaidi huku ikiwajali wachezaji na viongozi.

Litatengengwa fungu la usajili kila kipindi cha usajili ili kuleta wachezaji watakaoisaidia Simba katika michuano ya ndani na nje ya nchi.

Hayo machache ambayo yanaelekea kufanyika hivi sasa ila kuna makubwa yanakuja na kila mpenzi na mshabiki wa Simba atakuwa na furaha.

Azania Post

Updated: 20.06.2018 13:05
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Hemedi Saidy 2018-06-20 14:42:03

Isiwe maneno sasa ni muda wa vitendo zaidi Kama Kweli basi Natoa Big up!

Avatar
Onesmo y mgullo 2018-06-20 13:22:35

I like it

Avatar
Rajabu waziri 2018-06-20 13:49:48

Kila la heri tunahitaji vitendo zaidi siyo maneno mengi

Avatar
Benjamin daud 2018-06-20 13:55:21

Tunaomba ahadi alizo toa azitimize tutafurahi sana

Avatar
NSABI ADIPUNAGA 2018-06-20 16:14:34

Mbona habari haina details, inaonekana ni ya kuungaunga hii habari

Avatar
Bin Dibwe 2018-06-21 13:15:17

Safi sana

Avatar
SUMUN 2018-06-23 22:12:25

I will enjoy more

Avatar
Alfred Faustine 2018-06-29 19:59:03

Hongera SIMBA MPYA: MO ' Ndo habar ya mjin...