Huyu ndiye Mtanzania atakayecheza Kombe la Dunia mwaka huu

Baba yake ni mzaliwa wa Tanga na mama yake ni raia wa Denmark

Huyu ndiye Mtanzania atakayecheza Kombe la Dunia mwaka huu

Baba yake ni mzaliwa wa Tanga na mama yake ni raia wa Denmark

05 June 2018 Tuesday 12:38
Huyu ndiye Mtanzania atakayecheza Kombe la Dunia mwaka huu

Na Amini Nyaungo

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania wa damu kucheza kombe la dunia mwaka huu, japokuwa hatokuwa na timu ya taifa la baba yake yaani Taifa Stars.

Baba wa Yussuf Paulsen ni Mtanzania ambaye alikuwa anafanya kazi Bandarini ambapo alikuwa anasafirisha katika meli kutoka Afrika kuelekea Denmark ambapo ndipo alipokutana na mama wa mchezaji huyo.

Hivyo mama yake ni mzungu raia wa Denmark lakini baba yake ni Mtanzania wa kuzaliwa na alifariki dunia wakati mchezaji huyo akiwa na umri wa miaka 6 pekee. Nyota huyo, ambaye anacheza katika ligi kuu ya Ujerumani aliwahi kuja Tanzania mwaka juzi wa 2017.

Baada ya muda mrefu alikuja Tanzania mwaka 2016 kuja kuiona familia yake mkoani Tanga, na kuweza kukutana na ndugu zake.

Yussuf Yurary Poulsen anacheza RB Leipzig ya ligi kuu ya Ujerumani maarufu kama Bundesliga, akiwa kama mshabuliaji na amefunga magoli 37 katika jumla ya michezo 156.

Kocha wa timu ya taifa ya Denimark Åge Hareide amemuita mchezaji huyo kuwa miongoni mwa wachezaji 23 watakaokipiga katika kombe la Dunia litakaloanza june 14 huko nchini Urusi.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.