Ibrahim Ajib 'ashikwa uchawi' taifa

Ibrahim Ajib 'ashikwa uchawi' taifa

01 October 2018 Monday 07:40
Ibrahim Ajib 'ashikwa uchawi' taifa

Ofisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara, ameamua kufunguka kuhusiana na namna kiungo wa Yanga, Ibrahim Ajib namna alivyoanzisha mpira kwa kuutoa nje.

Ajib alianzisha mpira huo kwa kuutoa nje baada ya Mwamuzi wa kati, Jonesi Rukiya kupuliza filimbi kuahsiria mwanzo wa dakika 45 za kwanza katika mechi dhidi ya watani zao wa jadi Simba.

Kitendo hicho kimemshangaza zaidi Manara akieleza kuwa hajawai kuona popote pale duniani katika mchezo wa soka kwa mchezaji kuanzisha mpira kwa kuutoa nje.

Manara ameeleza kuwa anajua ni vigezo na masharti ambayo alipewa mchezaji huyo jambo ambalo lilipelekea kuutoa mpira nje badala ya kumuanzishia mwenzake.

"Ibrahim Ajibu Migomba dunia inajua na wewe unajua namna nnavyoikubali miguu yako, na kwangu mim kando ya Kakolanya wewe ndiyo manusura yao leo, maana hapo si bahati mbaya, ni yale masharti na vigezo"

"Nimeangalia mechi za mpira na kwenye TV zaidi ya elfu kumi sijawahi ona hii ya leo, napingana hapa iwekwe kwenye Guinness World Records Book". aliandika.

Aidha, Manara ameeleza kuwa hajawahi kuamini uchawi katika mpira kutokana na timu yake ilivyopata nafasi nyingi dhidi ya watani zao lakini ikashindwa kufunga huku ikiongoza kwa takwimu zote uwanjani.

"Sijawahi kuamini Uchawi katika mpira, lakini huku kwetu upo na unafanya kazi, wameshinda wao 0-0" aliandika kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Katika mchezo huo, Simba na Yanga zilienda sulluhu ya kutofungana (0-0) ikiwa ni mechi ya kwanza kwa timu hizo mbili kukutana msimu huu. 

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.