Ibrahim Ajibu, TP Mazembe kimeeleweka

Taarifa ya TP Mazembe kwa klabu ya Yanga ya Mei 16, 2019 inaeleza kusudio lao la kumsajili Ajibu kama mchezaji huru

Ibrahim Ajibu, TP Mazembe kimeeleweka

Taarifa ya TP Mazembe kwa klabu ya Yanga ya Mei 16, 2019 inaeleza kusudio lao la kumsajili Ajibu kama mchezaji huru

22 May 2019 Wednesday 09:12
Ibrahim Ajibu, TP Mazembe kimeeleweka

Na mwandishi wetu, Dar es salaam

NI wazi sasa mchezaji nguli na kipenzi wa timu ya Yanga, Ibrahim Ajibu anatakiwa na TP Mazembe ya DRC Congo. 

Hatua hiyo inawekwa hadharani ikiwa ni siku mbili tu tangu bilioni na mmiliki wa TP Mazembe Moise Katumbi kurejea DRC Congo baada ya kukaa uamishoni kwa takribani miaka mitatu kufuatia mgogoro wake wa kisiasa na  rais  mstaafu wa nchi hiyo, Joseph Kabila.  Katumbi alikuwa gavana wa jimbo lenye utajiri wa madini la Katanga.

Tayari TP Mazembe ameshaanza utaratibu wa kumsajili mchezaji huyo ambaye hivi karibuni ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania itakayoshiriki michuano ya Afrika (AFCON) mwezi Juni. Michuano itayovulumishwa nchini Misri. Katika mashindano hayo Taifa Stars imepangwa kundi moja na timu ya Senegal, Algeria na Kenya

Taarifa ya TP Mazembe kwa  klabu ya Yanga ya Mei 16, 2019 inaeleza kusudio lao la kumsajili Ajibu kama mchezaji huru kufuatia mkataba wake kumalizika mwezi Juni 30, 2019. Na kwamba mazungumzo ya awali yameshafanyika na  mwezi  Julai, 2019 mambo yatakamilika. 

TP Mazembe imekuwa ikimfuatilia mchezaji huyo kwa muda mrefu na sasa tuseme yametimia.

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu ni miongoni mwa wachezaji wa tanzania waliowahi kuchezea TP Mazembe na kupata mafanikio ikiwemo kuchukua ubingwa wa Afrika

Updated: 23.05.2019 09:13
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
Joseph Kamongo 2019-05-28 09:02:55

Ahaa

Avatar
Swagger Boy 2019-05-31 17:05:55

Mwaambien Ajbu Asi Kataee Bahat Iyo Yanga Hamna K2

Avatar
Iddi 2019-06-05 22:39:38

Huko Bech 2

Avatar
meka boy 2019-06-07 16:32:13

ajib kaza buti bhana acha mamb meng

Avatar
mohamedi okono 2019-06-20 21:57:01

simba mfanye usajiri wa wafungajitu viungo wanatosha ira Ajibu Tp mazembe m,awezi bora ajenamungo

Avatar
mohamedi okono 2019-06-20 22:04:51

simba kahatafundi msainishen yangawaisome

Avatar
mohamedi okono 2019-06-20 22:09:29

ajibu kwendamazembe sawanakujenda daraja baharini

Avatar
mohamedi okono 2019-06-20 22:15:07

ajibu,kwendamazembe sawa na kujenga daraja baharini