Ismail Aden Rage atoa tamko baada ya kipigo cha Mbao FC

Ismail Aden Rage atoa tamko baada ya kipigo cha Mbao FC

22 September 2018 Saturday 10:02
Ismail Aden Rage atoa tamko baada ya kipigo cha Mbao FC

Baada ya kupoteza mchezo wa ligi juzi Alhamis dhidi ya Mbao FC, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amewataka mashabiki wa timu hiyo kushusha presha chini.

Rage ameeleza kuwa ifikie hatua wanasimba waelewe kuwa katika mpira hakuna timu inayoshinda siku zote bali kuna siku lazima ipoteze ama iende suluhu.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya mashabiki wa timu hiyo kuanza kuutupia lawama uongozi kutokana na kupoteza jambo ambalo liliepekea kutupiwa chupa kwa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Haji Manara.

Rage amewaomba wanasimba kushusha presha chini na kuchukulia kuwa ni hali ya mchezo hivyo ni vema wakatuliza munkari kwa kuwa timu ina kikosi kizuri.

Kiongozi huyo amewashauri wanasimba wote kuwa wapole kwani anaamini kikosi kitakuja kufanya vema zaidi siku uzoni kutokana na namna ilivyosajili.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.