Jose Mourinho: Ronaldo anatisha!

Jose Mourinho: Ronaldo anatisha!

13 September 2019 Friday 06:26
Jose Mourinho: Ronaldo anatisha!

KOCHA mbwatukaji, Jose Mourinho amesifia uwezo wa mshambuliaji Christiano Ronaldo akisema ni mpachikaji wa mabao ambaye hana mfano.

Mourinho ambaye kwa sasa ni mchambuzi wa soka kupitia kituo cha Skysport anasema uwezo wa staa wa Juventus Ronaldo ni wa hali ya juu na kwamba hata akifisha umri wa miaka 50 uwezo wake wa kufumania nyavu utabaki pale pale.

Atoa maoni yake hayo ikiwa ni siku chache baada ya Ronaldo kufunga magoli 4 katika mchezo wa kuwania kufuzu Euro 2020 dhidi ya Luthania.

‘‘Hata wakati atakapostaafu soka na kufikisha umri wa miaka 50 akialikwa katika mechi za ‘legends’ atafunga tu,’’ anasema Jose ambaye ni kocha wa zamani wa Man United na Real Madrid

“Ameweka alama ni mtu fulani anayefikiria kuhusu kushinda na kufanya zaidi kwa ubora, ndio maana huwa sishangazwi kwa anachokifanya kila siku, wakati atakapokuwa na umri wa miaka 50 atakuwa nyumbani na FIFA watakuwa wanamualika katika mechi za ma-legends, atacheza na kufunga magoli, nina uhakika itakuwa kama hivyo.

Wikendi iliyopita Cristiano Ronaldo ambaye ni Mreno aliiingia kwenye vichwa vya habari baada ya kuweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Ulaya kufunga magoli 90 katika michezo ya kimataifa ya timu za taifa akifuatiwa na Ferenc Puskas mwenye magoli 84 akiwa amestaafu soka toka 1962

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.