banner68
banner58

Juuko, Niyonzima wapewa masharti Simba

Juuko, Niyonzima wapewa masharti Simba

12 September 2018 Wednesday 18:26
Juuko, Niyonzima wapewa masharti Simba

Wachezaji wa Simba, Juuko Murshid raia wa Uganda na Mnyarwanda Haruna Niyonzima, wamerudishwa kwenye timu lakini kwa makubaliano maalumu.

Wachezaji hao ambao wako jijini Dar es Salaam, walikaa kikao 'kizito' na Kaimu Rais wa Simba, Salim Abdallah 'Try Again' na kufanya makubaliano hayo.

Wachezaji hao ambao hawakuwa pamoja na timu kwa kipindi kirefu kutokana na madai ya utovu wa nidhamu. Sehemu ya masharti yao ni kwenda sawa na matakwa ya klabu.

Wachezaji hao hawajaanza mazoezi ya pamoja na wenzao na wanatarajiwa rasmi kesho Alhamisi ambapo watafanya pamoja na kikosi cha pili ambacho kitabaki jijini Dar es Salaam na kocha msaidizi, Mrundi Masoud Djuma.

Baadhi ya wachezaji ambao ni 20, pamoja na benchi la ufundi chini ya Kocha Mkuu, Patrick Aussems isipokuwa Djuma, wataondoka kesho kwa usafiri wa ndege kwenda Mtwara.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
mrisho moka 2018-09-13 16:16:50

tunamuhitaji sna juuko murshid....wawa na nyoni mmojawapo akipata majeruh...sion tegemeo lingine lenye uhakika zaidi ya juuko...bukaba na mlipili sio wa uhakika kam juuko