Kagere amleta Kahata Simba

Simba yaingia makubaliano na Kahata, aitaka kumalizana na Gor Mahia

Kagere amleta Kahata Simba

Simba yaingia makubaliano na Kahata, aitaka kumalizana na Gor Mahia

05 July 2018 Thursday 09:32
Kagere amleta Kahata Simba

Kiungo wa Gor Mahia Francis Kahata tayari ameshaeleza nini kifanywe na mabingwa hao wa ligi kuu Tanzania Bara ili kuweza kupata saini yake, kama ilivyokuwa kwa mwenzake, Meddie Kagere.

Kahata ambaye ni raia wa Kenya, hivi sasa yupo jijini Dar es Salaam na timu yake ya Gor Mahia ambayo inashiriki mashindano ya vilabu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati maarufu kama Kombe la Kagame ambapo bingwa wake anapewa shilingi milioni 68.

Hivi karibuni, Simba ilikamilisha usajili wa mshambuliaji Meddie Kagere kutoka Gor Mahia ambaye alikuwa akicheza katika kikosi cha kwanza cha Gor Mahia na kuipa mafanikio makubwa timu hiyo.

Chanzo ndani ya klabu ya Simba kinasema kuwa mazungumzo baina ya Simba na Kahata yamekamilika, huku ikielezwa kwamba fedha za usajili zitakuwa ni shilingi milioni 120 huku mshahara wa kila mwezi kwa mchezaji huyo kuwa dola 5,000 (sawa na shilingi 11,363,000).

“Baada ya kumalizana katika mazungumzo hayo, Kahata akawaambia Simba kwamba wazungumze na viongozi wa timu yake, iwapo watafikia makubaliano, yeye hana shida na atakuwa tayari kujiunga na wekundu hao wa Msimbazi, lakini iwapo ikishindikana basi kwa kuwa bado ana mkataba nao,” kilisema chanzo.

Kagere mwenyewe amewataka Simba kufanya kila linalowezekana kumnasa mchezaji huyo kwani anafahamu uwezo wake.

“Kama mambi ni hivyo, Simba wamsajili tu kwani ni mchezaji mzuri, ninamfahamu kwani nimecheza nae. Kama akija basi tutakuwa na timu nzuri sana,” amesema Kagere.

Updated: 05.07.2018 09:34
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.
Avatar
J4 Suleiman 2018-07-20 22:22:21

Acheni simba kusajili mchezaji huyo kisa kagere kwani pengine kagere anamtafutia dili tu.

Avatar
athuman aka nyeuc 2018-08-06 13:58:19

kama anamkataba fanyeni mjango mwingine

Avatar
razack mkungu 2018-11-10 21:42:34

fanyen juu chn kwan xmba huyo kahata ni bonge la mchezaji

Avatar
maltin shitindi 2019-06-03 10:40:56

bonge la fundi

Avatar
Thobi 2019-06-28 21:19:50

Hayo yote yanafanywa na kamati ya usajili. Iacheni kamati ifanye kazi yake