banner68

Kamati TFF yajitosa suala la uchaguzi Simba

Kamati TFF yajitosa suala la uchaguzi Simba

12 July 2018 Thursday 10:37
Kamati TFF yajitosa suala la uchaguzi Simba

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania itakaa wiki ijayo kujadili suala la uchaguzi Simba ili kupata viongozi wapya ambao wataiongoza klabu hiyo kwa mujibu wa katiba inayotambulika.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Wakili Revocatus Kuuli, ameeleza wao kama kamati watakuwa na kikao wiki kesho kwa ajili ya kujadili suala la uchaguzi wa Simba kutokana na viongozi waliopo hivi sasa muda wao wa utawala unamalizika mwezi huu.

Kamati hiyo imeamua kufikia maamuzi hayo kutokana na kuitambua katiba ya mwaka 2014 kuwa ndiyo inayopaswa kufuatwa na Simba tofauti na ya sasa ambayo ipo kwa msajili iliyo na mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshwaji wa klabu.

Ikumbukwe viongozi wa Simba walituma barua kwenda TFF wakiomba mchakato wa kusajili katiba yao ukamilike ndipo watakuja kufanya uchaguzi hapo baadaye ili kuwapata viongozi wapya.

Katiba ya Simba iliyopo kwa msajili hivi sasa inamtaka mgombea atakayewania kiti cha Urasi awe na Shahada tofauti na ilivyokuwa awali ambapo ilikuwa inaruhusiwa hata ukiwa na cheti cha kidato cha nne.

Updated: 12.07.2018 10:48
Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.