Kaseja akabidhiwa 'bingo' yake

Kaseja akabidhiwa 'bingo' yake

10 September 2019 Tuesday 06:36
Kaseja akabidhiwa 'bingo' yake

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

PAUL Makonda ambaye ni mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ametimiza ahadi yake ya kumpa zawadi ya Milioni 10 golikipa, Juma Kaseja baada ya kumtangaza kama nyota wake wa mchezo kati ya Tanzania dhidi ya Burundi, mechi iliyomalizika kwa Tanzania kushinda kwa penati 3-0.

Mechi hiyo ilichezwa kwa dakika 120 na kumalizika kwa sare ya kufungana magoli 1-1, goli la Tanzania likifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30 huku la Burundi likifungwa na Feiston dakika za nyongeza kabla ya kwenda mapumziko, mikwaju ya penati ndio iliamua timu ipi isonge mbelee baada ya kuwa na ‘aggregate’ ya 2-2.

Ndipo Kaseja alifanikisha Taifa Stars kupata ushindi wa penati 3-0 na kuingia hatua ya makundi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, Kipa huyo wa timu ya KMC alikuwa shujaa wa mchezo huo baada ya kucheza penati ya kwanza iliyoleta nguvu kwa Taifa Stars na kuwadhoofisha Burundi.

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.