banner68
banner58

Kaseja ampotezea Okwi, Simba ikifa 1-0 kwa mara ya kwanza

Kaseja ampotezea Okwi, Simba ikifa 1-0 kwa mara ya kwanza

19 May 2018 Saturday 16:47
Kaseja ampotezea Okwi, Simba ikifa 1-0 kwa mara ya kwanza

Na Amini Nyaungo

Baada ya michezo 28 bila kupoteza hatimaye Simba yakubali kichapo cha goli 1-0 kutoka kwa Kagera Sugar katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo haukuwa rahisi mbele ya Rais John Pombe Magufuli na kuifanya Simba ipoteze kwa mara ya kwanza katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Hata hivyo Simba ilifanikiwa kupata penati katika dakika za majeruhi, lakini penati hiyo ilipanguliwa na aliyekuwa kipa wa Simba Juma Kaseja.

Juma Kaseja imeonekana kama aipotezea Simba baada ya kupangua penati ya Emanuel Okwi na kuweka historia nzuri ya kuifunga Simba timu yake ya Kagera.

Hii imetokea kama ilivyokuwa Barcelona baada ya kukubali kichapo cha magoli 5-4 dhidi ya Levante.

Azania Post

Comments
Avatar
Your Name
Post a Comment
Characters Left:
Your comment has been forwarded to the administrator for approval.×
<strong>Warning!</strong> Will constitute a criminal offense, illegal, threatening, offensive, insulting and swearing, derogatory, defamatory, vulgar, pornographic, indecent, personality rights, damaging or similar nature in the nature of all kinds of financial content, legal, criminal and administrative responsibility for the content of the sender member / members are belong.